Breaking News

Your Ad Spot

Nov 19, 2010

VODACOM TANZANIA YAWAKABIDHI MAGARI YAO LEO WASHINDI 100 WA SHINDA MKOKO NA VODACOM

Miongoni mwa mikoko 100 waliyokabidhiwa washindi leo 
Mkurugenzi wa Biashara na Masoko wa kampeni ya kuuza magari ya Hyundai, Irene Kwimbere akimkabidhi hati ya shukurani, Mkurugenzi  Mtendaji wa Kampuni ya Simu za mkononi ya Vodacom Tanzania, Dietlof Mare kabla ya kukabidhi magari 100 kwa washindi 100 wa 'shinda mkoko na vodacom', leo kwenye viwanja vya Mlimani City, Dar es Salaam. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Dietlof akiwa na Mwamvita Makamba wa Vodacom 
Dietlof na Ofisa wa Masuala ya habari wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu wakimpongeza mmona wa washindi,  Maijo Hamisi (28) baada ya Dietlof kumkabidhi funguo ya gari lake la ushindi. 
Hamisi akishangilia kwa furaha baada aya kukabidhiwa funguo za gari lake aina ya Hyundai i10 
Hamisi ambaye ni msimamizi wa meza ya mchezo wa pool akifurahia gari lake baada ya kuingia ndani 
Mjasiriamali Theonestina Kyagala mkazi wa Kigamboni akiwa katika gari lake, akiwa ni miongoni mwa washindi 100 waliokabidhiwa gari zao leo 
Meneja Mkuu wa Dodoma Hotel, Wellingtone Maleya, naye ni miongoni mwa washindi 100 walioshinda mikoko ya Vodacom. Pichani, akiwa katika gari lake baada ya kukabidhiwa leo katika sherehe hiyo. 
Na huyu Dada wa benki ya NBC , Yolanda Aloyce pia alikabidhiwa mkoko kati ya hao 100, ndiyo hapa anaujaribu baada ya kukabidhiwa katika sherehe hiyo leo. 
BAADHI ya washindi 100 wa 'shinda mkoko na Vodacom' wakiwa kwenye sherehe hiyo, huku wakipata 'bite' kidogo kidogo kabla ya kukabidhiwa mikoko yao.
=======================================
HABARI KAMILI
KAMPUNI ya simu ya mkononi ya Vodacom Tanzania kupitia promosheni yake ya 'Shinda Mkoko' leo imekabidhi magari 100 aina ya Hyundai i10 kwa washindi wake ikiwa ni ishara ya kukamilika kwa shindano hilo lilianza rasmi Agosti 2 mwaka huu.

Katika promosheni hii iliyochukua takribani siku 100 kila siku mteja mmoja wa Vodacom Tanzania alizawadiwa gari ambapo hadi bahati nasibu hii inafikia mwisho wake ikiwa ni maadhimisho ya miaka kumi ya utoaji huduma wa kampuni hiyo nchini tayari jumla ya washindi 100 walikwishapatikana.

 Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi magari hayo Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Dietlof Mare alisema kwa kutambua umuhimu wa jamii inayofanya nayo biashara kampuni yake iliona irudishe kiasi cha faida wanayoipata kwa wananchi ili kiwasaidie.

        "Katika kusherehekea maadhimisho haya ya utoaji huduma zenye mafanikio kwa wateja wetu na jamii kwa ujumla, tumeona tutumie fursa hii ya kumbukumbu ya miaka kumi ya utendaji wa Vodacom Tanzania kwa kurudisha faida iliyopatikana kwa wateja wetu," alisema Mare.

Akifafanua alibainisha kuwa katika kipindi cha miaka 10 ya utoaji huduma nchini Vodacom imejiwekea utaratibu wa kutoa huduma bora tena za kipekee na uanzishwaji wa promosheni mbalimbali kwa lengo la kuiwezesha na kuinua kichumi jamii ya Watanzania.

"Licha ya kuwazawadia magari 100 wateja wetu mbalimbali, pia mtandao wetu una wateja takribani milioni 6 waliojiunga kwenye huduma ya kutuma na kupokea fedha ya M-Pesa iliyoenea kote nchini," alisema.

Naye Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni hiyo Ephraim Mafuru alisema shindano hilo liliwahusisha wateja wote wa kampuni hiyo nchini waliofika kutoka maeneo tofauti nchini kupokea magari yao.

Aidha aliongeza kwamba washindi katika promosheni hiyo walipatikana baada ya kuwa na pointi nyingi walizojikusanyia ambazo zilichezeshwa kwenye droo ili kumpata mshindi wa promosheni hiyo kila ilipochezeshwa.

"Wakati promosheni inaendelea baadhi ya watu walidai tusingeweza kugawa magari haya 100 kwa kuwa ni wababaishaji, lakini kupitia bodi ya michezo ya kubahatisha nchini (TGB) leo tumetimiza lengo letu na kuwazawadia washindi magari yao," alisema Mafuru.

Kwa upande wake Meneja Mtendaji wa New Dodoma Hoteli Wellingtone Maleya alisema hafla hiyo imeondoa dhana kwamba wateja walikuwa wanapeleka fedha Vodacom ili watangazwe washindi hali ambayo imedhihirika kwamba ni uzushi.

"Leo tunashuhudia wateja wa matabaka tofauti wakikabidhiwa magari yao, wengine ni mameneja, akina mama wa nyumbani na hata shamba boy. Kama ingekuwa kupeleka hela Vodacom ndio kushinda leo tungekutana tunaojiweza watupu hapa," alisema Maleya.

Hyundai i10 ni gari inayohimili mazingira ya mijini (hatchback) ambayo imetengenezwa na Kampuni ya magari na mitambo ya Hyundai Motor Company, na lilizinduliwa rasmi nchini Oktoba 31, mwaka 2007.

Gari hiyo ya gharama nafuu ni rahisi kuihudumia kwani inatumia kiwango kidogo cha mafuta ikiwa pia tofauti na magari mengine ambayo unapoyatumia unajisikia raha na kukuweka huru.

1 comment:

  1. [url=http://LOVEINABOTTLE.info/?p=71]free games online[/url]

    ReplyDelete

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages