Breaking News

Your Ad Spot

Jan 5, 2011

STARS KUFUNGUA DIMBA NA MAFARAO KATIKA MICHUANO YA NILE

TIMU ya Taifa Stars inashuka dimbani leo katika mechi ya fungua dimba ya mashindano ya kombe la Nile, kwa kukwaana na wenyeji Misri 'Mafarao'.

   Wakati Stars ikipepetana na wenyeji, Uganda na Burundi nazo zitakuwa na kibarua katika mechi nyingine aambayo pia inachezwa leo.
     Stars inashuka dimbani ikiwa na kumbukumbu ya kipigo cha mabao 5-1 ilichopata mwaka jana, dhidi ya Mafarao hao katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa.

Michuano hiyo inashirikisha timu saba ambazo ni pamoja na Stars, Burundi, Uganda, Sudan, Congo DRC na wenyeji Misri.

Bingwa katika michuano hiyo ataondoka na kitita cha dola 176,000 za Marekani, ambazo ni kama sh. milioni 260 hivi za Kitanzani.


No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages