Breaking News

Your Ad Spot

Feb 23, 2011

IDADI YA WANAWAKE WASIOJUA KUSOMA HAIJASHUKA-MIGIRO




NA MWANDISHI MAALUM,NEW YORK
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dk. Asha-Rose Migiro

 Imeelezwa kuwa wanawake ni theruthi mbili ya watu wote wazima wasio jua kusoma. Na kwamba takwimu hizo hazijaonyesha dalili ya kushuka kwa takribani miaka ishirini sasa.


Hayo yameelezwa na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dkt. Asha-Rose Migiro wakati alipokuwa akifungua mkutano wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu Hali ya Wanawake ( CSW). Ufunguzi wa mkutano huo wa wiki mbili umefanyika siku ya Jumanne hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa New York.


Ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mkutano huo, unaongozwa na Mhe. Ummi Ally Mwalimu (MB),Naibu Waziri, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto.


Akiuhutubia umati wa wajumbe kutoka nchi wanachama 192 wa UM, Migiro anaeleza kuwa licha ya kwamba uwekezaji katika elimu hususani kwa wanawake na watoto wa kike ni jambo lisilo na ubishi, bado kundi hilo la jamii limeendelea kuachwa nyuma.


Anasema Migoro, “ wakati mkiwa mmechagua elimu kama dhima kuu la mkutano wenu. Na wakati tunajadili hali ya wanawake, ni vema mkatambua kwambaTheruthi mbili ya watu wazima wasio jua kusoma ni wanawake. Na takwimu hizi hazijabadilika kwa kipindi cha miaka 20.


Kwa hiyo anasema Naibu Katibu Mkuu, hakuna jambo jema kama uwekezaji katika elimu, manufaa yake ni makubwa na ni mengi. Elimu sit u kwamba ni ufunguo muhimu katika ukuaji wa uchumi. Lakini ni nyezo muhimu sana katika uwezeshaji wa mwanamke.


Akabainisha kuwa nchi nyingi zimejidhatiti sana katika kuhakikisha kwamba zinafikia lengo la kila mtoto mwenye umri wa kwenda shule na bila ya kujali jinsia yake anapata fursa hiyo.


Hata hivyo anasema kuwa pamoja na jitihada hizo kumnufaisha mtoto wa kike, lakini bado kunachangamoto kubwa wenye ubora wa elimu inayotolewa.


“ Bado ubora wa elimu inayotolewa hususani katika nchi zinazoendelea haujaendana na kasi ya kuandikishaji wa watoto. Watoto wengi wanamaliza shule wakiwa hawana ujuzi na maarifa ya kusoma wala kuhesabu” anabainisha Migiro.


Kama hiyo haitoshi, Naibu Katibu Mkuu anaeleza zaidi kwa kusema, uwakilishi wa wanawake katika Nyanja za sayansi, teknolojia ,elimu na ajira bado ni wa kiwango cha chini.


“ kwa ufupi ni kwamba hawapati ujuzi na maarifa yatakayowawezsha kushindana katika soko la ajira la dunia ya leo: anasisitiza Naibu Katibu Mkuu.


Akawataka wajumbe wa mkutano huo, kuutumia mkutano huu kujadiliana na kubadilishana mawazo na hatimaye kutoka na majibu ya mambo ya msingi ambayo bado yanaendelea kuwa kikwazo kwa maisha bora na maendeleo ya mwanamke.


Aidha amewataka wajumbe hao kuendeleza harakati za kumkomboa mtoto wa kike na vilevile kupinga ukatili dhidi ya mwanamke.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages