Breaking News

Your Ad Spot

Feb 18, 2011

MABOMU GONGO LA MBOTO LEO

WABUNGE Dk. Faustine Ndugulile (Kigamboni), Abasi Mtenvu (Temeke), Mussa Zungu (Ilala) na Makongoro Mahanga (Segerea) wakizungumza na Victoria Charles mkazi wa Pugu, ambaye amelazwa katika hospitali ya Amana, Ilala, Wabunge wa mkoa wa Dar es Salaam, walipotembelea waathiriwa wa mabomu ya Gongo la Mboto.

RAIS wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Sheni alizungumza na wabunge wa mkoa wa Dar es Salaam, nje ya wodi, baada ya kuwajulia hali waathiriwa wa mabomu ya Gongo la Mboto, leo 
Katibu Mkuu wa CCM, Yussuf Makamba, akizungumza na mmoja kati ya watoto waliopo katika kambi ya muda ya waathirika wa mambomu ya Gongo la Mboto, alipotembelea kambi hiyo leo. 
Watoto waliopo katika kambi hiyo wakipiga msosi leo mchana
Mwenyekiti wa CUF, Taifa, Profesa Ibrahim Lipumba (wapili kushoto) na ujumbe wake wakiambatana na Mganga Mfawidhi wa hospitali ya Amana, alipowasili katika hospitali hiyo kuwajulia hali majeruhi waliolazwa  
Kaimu Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, M. Sadiki, akizungumza na waathirika wa mabomu hayo waliopo kambi ya muda ya PTA, viwanja vya sabasaba 
Vyakula na vinywaji mbalimbali kwa ajili ya waathirika waliopo kambi ya muda 
Wadau wakimpa pole muathiriwa wa mabomu aliyelazwa hospitali ya Amana, Ilala
MWAKILISHI wa kampuni inayoandaa  kipindi cha maigizo cha simu ya mkononi katika kituo cha TBC, Elite Enterprenue 4 Africa,  Kethy Rupia (kushoto), akimkabidhi msaada wa vitu mbalimbali vikiwemo vyakula, Mratibu wa Msalaba Mwekundu mkoa wa Dar es Salaam, Grace Mawala, leo kwenye kambi ya muda ya wathirika wa mabomu ya Gongo la Mboto. (Picha  zote na  Chachandudaily.blogspot.com).

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages