Mbunge wa Viti Maalum (CCM). Vicky Kamata akisalimiana na Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa baada ya kuiba wimbo wake, wabla ya uzinduzi wa albamu hiyo. Kulia ni Mchungaji Kiongozi wa Kanaisa la Ufufuo na Uzima, Josephati
Lowassa akieleza yake machache na kuongoza kuimba wimbo wa kumtukuza Mungu, kabla ya kuzindua rasmi albamu hiyo na kuendesha harambee ya uchangiaji fedha kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha watoto yatima Kiluvya.
KIONGOZI wa Bendi ya muziki wa Injili ya Mwanamapinduzi, Mchungaji Maximilian Machumu, akimkabidhi CD, DVD NA Kanda za albamu ya 'Bonde la kukata maneno', Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, wakati wa uiznduzi wa albamu hiyo, uliofanyika juzi, katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam. Lowassa ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo, alichangia sh. milioni moja. Katikati ni, Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima (GCTC Josephat Gwajima.
Lowassa akinadi CD na DVD za albamu hiyo. Kushoto ni Max
Max na waimbaji wa bendi yake, wakiimba kwa hamasa baada ya uzinduzi wa albam yenyewe .
-------------------------
STORI KIDOGO
BENDI ya muziki wa injili ya Mapinduzi, imevuna jumla ya sh. milioni 40, katika uchangishaji fedha uliosimamiwa na Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa, kwenye uzinduzi wa albamu ya 'bonde la kukata maneno' juzi katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Lowassa alisema, umefikia wakati ambao Watanzania sasa waachane na malumbano na kutupiana maneno yasiyojenga, dala yake, wajikite katika kufanya mambo yenye tija ikiwemo kumcha Mungu ambaye ndiye mwenye uwezo katika kila jambo.
Mapema, Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Rudisha Music, iliyoaandaa uzinduzi wa albamu hiyo, Frederick Fussi alisema, lengo ni sehemu ya pamato ikiwa ni pamoja na mnada wa DVD, VCD na Kanda yatatumika kujenga kituo hicho cha yatima ambapo ujenzi huo umekadiriwa kuhitaji sh. milioni 120.
Uzinduzi uliambatana na burudani za sarakasi na tumbuizo za muziki wa injili kutoka kwa Kamata na vikundi kadhaa vya muziki huo na kufuatia na Maximilian mwenyeye na kundi zima la Mapinduzi, kupanda jukwaani kuzindua rasmi almabu yao, hatua iliyosababisha mamia ya watu waliohudhuria kupata burudani murua kutokana na umahiri ulioonyeshwa.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269