Breaking News

Your Ad Spot

Mar 16, 2011

SHAABAN DEDE AACHIA NGAZI SIKINDE, ARUDI MSONDO BAND

Mwanamuziki mahiri, mwandamizi wa bendi ya Siikinde, Shaaban Dede, ametangaza kuihama bendi hiyo, na kurejea Msondo Band 'Baba ya Muziki' ambako alikuwwa miaka ya 80 kabla ya kujiunga na Sikinde.

Akizungumza na kipindi cha michezo cha Radio One, jana jioni, Dede alisema, ameamua kwenda Msondo si kwa sababu ya kukimbia matatizo yaliyopo Sikinde, ila ni kwa sababu tangu akiwa katika bendi hiyo badi Msondo ilikuwa katika damu yake.

Dede ambaye ni mahiri kwa utunzi wa nyimbo zenye msiismko wa aina yake, amesema anatarajia kufanya mambo makubwa akaiwa Msondo.

Hatua ya kurejea kwa mwanamuziki huyo ndani ya  Msondo, huenda kukarejesha vionjo vya zama za bendi hiyo, ingawa ameingia huku baadhi ya wanamuziki wakiwa hawapo kutokana na kukumbwa na kifo.

Pengine kuingia Msondo, utawezesha Dede kuziba walau kidogo pengo la wanamuziki mahiri ndani ya bendi hiyo ambao wamefariki kwa nyakati tofauti, akiwemo aliyekuwa mwimbaji matata, Tx Moshi William na wengine kibao.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages