.

JK AAHIRISHA KUTOA HOTUBA YAKE YA MWEZI LEO; SASA KUITOA KWENYE MEI MOSI MJINI MORO

Apr 30, 2011

"Hotuba ya mwisho wa mwezi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, kwa mwezi huu wa Aprili, iliyokuwa itolewe usiku wa leo, Jumamosi, Aprili 30, 2011, haitakuwepo,  kama ilivyo kawaida kwa kila mwezi.
Badala yake, Mheshimiwa Rais ameamua kutoa ujumbe wake wa mwezi wa Aprili kwa wananchi kupitia hotuba yake ya atakayotoa kesho katika Sherehe za maadhimisho ya Sikukuu ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi),  zitakazofanyika kitaifa kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro ambako atakuwa mgeni rasmi", ilisema taarifa ya Ikulu leo.

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช