.

MABADILIKO CCM; DODOMA YAENDELEA KURINDIMA, JK AZUNGUMZA NA SEKTRETARIETI MPYA YA CCM, AKUTANA NA WAFANYAKAZI MAKAO MAKUU YA CHAMA DODOMA

Apr 12, 2011

Mwenyekiti wa CCM ,Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikutana na Secretariet Mpya ya Chama cha Mapinduzi ofisini kwake makao makuu ya CCM mjini Dodoma leo mchana.Kushoto ni Makamu Mwenyekiti CCM bara Pius Msekwa,Wapili kulia ni Katibu mkuu moya wa CCM Wilson Mkama, Naibu katibu mkuu Zanzibar Vuai ali vuai,Katibu itikani na uenezi Nape Mnauye, na Katibu Organizesheni NEC Bi.Asha Abdullah Juma. 
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete(watatu kushoto), akimtambulisha katibu mkuu mpya wa CCM Bwana Wilson Mkama kwa wafanyakazi wa  Makao makuu ya CCM mjini Dodoma leo asubuhi.Wengine kutoka kushoto ni ni Naibu katibu mkuu Zanzibar Vuai Ali Vuai,Makamu wa CCM Bara Pius Msekwa, na wamwisho kulia ni naibu katibu mkuu John Chiligati .
Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete akizungumza na wafanyakazi wa makao makuu ya CCM mjini Dodoma leo.
Wanachama wa CCM walichaguliwa kuunda secrtarieti mpya  kutoka kushoto ni Mweka Hazina mpya wa CCM taifa Mwigulu Lameck Nchemba,Katibu Itikadi Mwenezi wa CCM taifa Nape Moses Mnauye,Katibu Organaizesheni NEC Bi Asha Abdullah Juma,Naibu Katibu mkuu CCM Zanzibar vuai Ali Vuai na January Makamba uhusiano Kimataifa(picha zote na Freddy Maro).
Katibu Mkuu mstaafu makamba akiwaaga wanachama baada ya kufanyika uchaguzi ulimchagua katibu mpya wa CCM Huko Dodoma,(kushoto) Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Dk Ali Mohamed Shein.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar na Mjumbe wa kamati Kuu Balozi Sif Ali Iddi,akimpongeza  Katibu Itikadi Mwenezi wa CCM taifa Nape Moses Mnauye, baada ya kuchaguliwa katika Mkutano wa  Halmashauri Kuu ya  CCM  Taifa,NEC Mjini Dodoma.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar na Mjumbe wa kamati Kuu Balozi Sif Ali Iddi,akimpongeza   Mweka Hazina mpya wa CCM taifa Mwigulu Lameck Nchemba,baada ya kuchaguliwa katika Mkutano  Halmashauri Kuu ya  CCM  Taifa,NEC Mjini Dodoma
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar na Mjumbe wa kamati Kuu Balozi Sif Ali Iddi,akimpongeza  Katibu Organaizesheni NEC Bi Asha Abdalla Juma,baada ya kuchaguliwa katika Mkutano wa Halmashauri Kuu ya  CCM  Taifa,NEC Mjini Dodoma. (Picha zote na Ikulu, Zanzibar).

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช