.

MAANDALIZI KILI TAIFA CUP; MARIPOTA WA MICHEZO WAPEWA SHAVU LA KUJIRUSHA SOUTH BEACH RESORT, KIGAMBONI

Apr 16, 2011

HABARI KATIKA PICHA
Waandishi wa habari za michezo wakiwa katika gari maalu kwenda kujilabu South Beach Resort
Baada ya kufika First ikawa kujipanga foleni kupiga menyu
Wakakaa foleni kila mmoja akapewa menyu kulingana na tumbo lake
Wakaketi na kuanza kupigwa msasa ili waifahamu vema michuano ya Kilimanjaro Taifa Cup, hasa ya mwaka huu itakavyokuwa
Baadhi yao wakawa wanabadilishana mawazo au akili wakati msasa ukiendelea kwenye ukumbi wa south Beach Resort
Habari zikawa zinaandikwa papo hapo kwa ajili ya kurushwa kwenye nyumba za habari kama mmoja wa watoa msasa alivyokuwa akisema akimaanisha Media house.
Meneja wa Kilimanjaro, Gerge Kavishe na Ofisa Habari wa TBL, Doris Malulu kukaw kuna jambo linawalazimu kuliangalia kwa msisitizo lakini bila kupuuza tabasamu zao
Timu ya wawezeshaji ilikuwa kamili, Kutoka kulia kwako ni Mtaalamu wa masualaya habari za PR kuto ka Exacutiv Solutions Ltd Benjamin Thopson, Meneja Biashara na Masoko wa TBL, David Minja, Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Oseah na Ofisa habari Doris
Doris akifungua pazia la upigaji msasa maripota hao kwa utambulisho
Minja akieleza umuhimu kuhusu TBL katika jamii ya Tanzania
Kavishe akitoa somo kuhusu nini maana, umuhimu, lengo la michuano ya Kili Taifa Cup na namna maandalizi ya mwaka huu yalivyoiva
Thompson akieleza namna nzuri ya kuandika au kuripoti habari za mdau kama TBL katika suala kama hilo la michuano ya Kili taifa Cup, kama mdhanini wa michuano hiyo
Katibu Mkuu wa TFF akijibu maswali ya washirki yaliyoelekezwa kwa TFF
Kisha manahodha wa timu mbili mahasimu za Simba na Yanga zinazodhaminiwa na Kilimanjaro Premium lager, wakapewa jezi kwa ajili ya kundi zilizoundwa chap chap kutokana na waandishi waliohudhuria shavu hilo.
Pambano likaanza. hapa Mzee wa Chachandu Daily, Bashir akimenyana vikali na shabiki wa simba Fadhili Akida,  Simba wakalala kwa bao 1-0
Moja ya hatari langoni mwa Simba ya Waandishi wa habari za michezo
Refa akimpa kadi nyekundu shabiki wa timu ya simba ya waandishi hao, Mwani.
Baada ya mechi manahodha wakabadilishana jezi
Na hii ndiyo nembo ya michuano ya Kili Taifa Cup mwaka huu, ambayo itarindima mwezi ujao kwa shavu kubwa la bia ya Kilimanjaro Premium Lager, ambao ndiyo pia wamesababisha shavu walilopata maripota hao0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช