Breaking News

Your Ad Spot

Apr 15, 2011

RAIS WA SOMALIA ATUA BONGO LEO


Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha mgeni wake
Rais Wa Somalia Sheikh sharif Sheikh Ahmed alipowasili
 nchini leo mrachana kwa zia ya kikazi ya siku mbili.

UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL 
PRESIDENT’S OFFICE,
      THE STATE HOUSE,
       P.O. BOX 9120,  
DAR ES SALAAM.
Tanzania
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Somalia, Mheshimiwa Sheikh Sharif Sheikh Ahmed amewasili nchini mchana wa leo, Ijumaa, Aprili 15, 2011, kwa ajili ya ziara rasmi ya siku mbili katika Tanzania.Rais Sheikh Ahmed na ujumbe wake wamepokelewa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere mjini Dar es Salaam na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ambaye ameongoza viongozi wengine wa Serikali kwa ajili ya mapokezi hayo yaliyopambwa kwa shamrashamra za ngoma za jadi na burudani nyingine.
Baadaye leo, Rais Kikwete anatarajiwa kufanya mazungumzo ya faragha na mgeni wake ambayo yatafuatiwa na mazungumzo rasmi ya Kiserikali kati ya Serikali za Tanzania na Somalia, Ikulu, Dar es Salaam.
Mazungumzo hayo rasmi yatafuatiwa na dhifa ya kitaifa itakayoandaliwa na Rais Kikwete kwa ajili ya mgeni wake.
Kesho, Rais Sheikh Ahmed atatembelea Ubalozi wa Somalia katika Tanzania ulioko Barabara ya Msasani, Oyesterbay na badaye atatembelea SUMA JKT katika eneo la Chang’ombe na pia kutembelea Magereza, Ukonga. Mgeni huyo ataondoka nchini kesho hiyo hiyo kurejea kwao.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
15 Aprili, 2011

PICHA ZAIDI ZA MAPOKEZI YA RAIS HUYO 
Rais Kikwete akiwa na mgeni wake Rais Sheikh sharif Sheikh Ahmed alipowasili nchini leo mrachana kwa zia ya kikazi ya siku mbili.
Sheikh sharif Sheikh Ahmed akikagua gwaride la vikosi vya Jeshi la wananchi wa Tanzania, alipowasili nchini leo mrachana kwa zia ya kikazi ya siku mbili.
Rais Kikwete na mgeni wake Sheikh sharif Sheikh Ahmed wakitazama ngoma mgeni huyo alipowasili nchini leo mrachana kwa zia ya kikazi ya siku mbili. (picha  zote na Freddy Maro). 

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages