.

MAKANDARASI WAZALENDO WAANZISHA UMOJA WAO

Apr 8, 2011

Mwenyekiti wa Chama cha Makandarasi Wazalendo Tanzania (ACCT), Andrew Mwaisemba akizungumza na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo) mjini Dar es Salaam, wakati uongozi ulipokuwa ukitangaza rasmi chama hicho. Kushoto ni, Katibu Mtendaji wa Chama hicho, Josper Mwandunga. 
Viongozi wa Chama Cha Makandarasi Wazalendo Tanzania, ACCT wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kuzindua chama hicho leo katika ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo) mjini Dar es Salaam. Walioketi kutoka kushoto ni,  Katibu Mtendaji Josper Mwandunga, Mwenyekiti wa chama hicho Andrew Mwaisemba na kulia ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Milton Nyerere.

1 Comments:

Anonymous said...

tunawaunga mkono makandarasi wazalendo. wajue bila kuungana hawatafika mbali. waangalie wenzao china na asia yote wana umoja na wanasaidiwa na serikali zao hivyo wameweza kupiga hatua kubwa. hata hivyo suala la rushwa litawaangusha, wajitahidi kulipiga vita ingawa vita hiyo ni ngumu kwani rushwa imekuwa kama kansa ktk tanzania

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช