.

RAIS KIKWETE NA RAIS SHEIN WAONGOZA HITMA YA HAYATI MZEE KARUME

Apr 7, 2011

Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein,(wa tatu kushoto), Rais Dk Jakaya Mrisho Kikwete, na viongozi wengine wakisoma hitma ya kumuombea dua muasisi wa Mapinduzi na Rais wa Kwanza wa Zanzibar Abeid Amani Karume, Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar.
Rais Jakaya Mrisho kikwete, akisalimiana na Mjane wa Mzee Abeid Amani Karume, baada ya  hitma ya kumbukumbu ya mzee huyo, Ofisi Kuu ya CCM. 
Viongozi na masheikh wakiwa ofisi Kuu ya CCM, Kisiwandui Zanzibar wakati wa hitima hiyo 
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka shada la maua kwenye kaburi la muasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar na Muungano wa Tanzania hayati Marehemu Mzee Abeid Karume katika bustani za ofisi za CCM Kiswandui Zanzibar leo asubuhi wakati wa maaadhimisho ya kumbukumbu ya kifo cha musaisi huyo. 
Rais wa Zanzibar Dk Ali MOhamed Shein,akiweka shada la mauwa katika kaburi la Muasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar Mzee Abeid Amani Karume
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete(kulia) Rais wa Zanzibar Dkt.Ali  Mohamed Shein (wapili kulia), Makamu wa pili wa SMZ Balozi Seif Iddi (watatu kulia), Spika Kificho wa Baraza la Wakilishi pamoja na Balozi  Ali Karume (kushoto) wakishiriki ibada ya kumuombea muasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar hayati Mzee Abeid Karume mjini Zanzibar leo asubuhi (Picha zote  na Freddy Maro na Ramadhan Othman )

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช