.

TBL YAJENGA KISIMA CHA SH. MILIONI 27 KITUNDA

Apr 17, 2011

Mkurugenzi wa Maji Mijini wa Wizara ya Maji, Mary Mbowe (kulia), akifurahia baada kuzindua juzi kisima cha maji cha  Mzinga A kilichojengwa kwa sh. milioni 27 zilizotolewa msaada na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), katika eneo la Kitunda Nyangasa, Dar es Salaam .Kutoka kushoto ni Mhandisi Ujenzi wa TBL, John Malisa, Mwenyekiti wa mradi huo, Rashid Nandonde na Meneja Miradi Maalumu wa TBL, Emma Orio.
Mkurugenzi wa Maji Mijini wa Wizara ya Maji, ambaye alimwakilisha Waziri wa Maji, Profesa Mark Mwandosya, Mary Mbowe (mbele), akitoka katika ofisi za kisima cha maji cha Mzinga A, Kitunda, Dar es Salaam, baada ya kukizindua juzi. Kisima chenye uwezo wa kutoa lita 30,000 za maji kimejengwa kwa gharama ya sh. milioni 27 zilizotolewa msaada na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Kutoka kushoto ni Mhandisi Ujenzi wa TBL, John Malisa  na Meneja Miradi Maalumu wa TBL, Emma Orio.
Meneja Miradi Maalumu wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Emma Orio, akimtwisha ndoo ya maji Mkazi wa Kitunda Nyangasa, Dar es Salaam, Pili Khamis wakati wa hafla ya uzinduzi wa kisima cha maji cha  Mzinga A, kilichojengwa kwa sh. milioni 27 zilizotolewa msaada na Kampuni ya bia Tanzania (TBL).
Mwenyekiti wa Mradi wa kisima cha maji cha Mzinga A, Kitunda Nyangasa, Dar es Salaam, Rashid Nandonde, akimtwisha  ndoo ya maji Mkazi wa eneo hilo, Catherine Mwatonoka, wakati wa hafla ya uzinduzi wa kisima hicho juzi, kilichojengwa kwa sh. milioni 27 zilizotolewa msaada na Kampuni ya bia Tanzania (TBL).
Mkurugenzi wa Maji Mijini wa Wizara ya Maji, Mary Mbowe (katikati), ambaye alimwakilisha Waziri wa Maji, Profesa Mark Mwandosya, akisindikizwa na Mhandisi wa Ujenzi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), John Malisa (kushoto) na Mjumbe wa Kamati ya Mradi wa Kisima cha Maji cha Mzinga A, Kitunda Nyangasa, Dar es Salaam, Josephine Msungwa akitoka kuzindua  mradi huo juzi.Kisima hicho kilichojengwa kwa sh. milioni 27 zilizotolewa msaada na TBL.

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ª