.

MSWADA WA KATIBA MPYA MZURI LAKINI UNA KASORO NYINGI: TLS

Apr 9, 2011

Rais wa Chama Cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) Francis Stolla, akitoa tamko la chama hicho kuhusu muswada wa sheria ya Katiba mpya, alipozungumza na waandishi wa habari, leo  kwenye Ofisi za TLS, mjini Dar es Salaam. Kulia ni Makamu wa Rais wa TLS Mpale Mpoki na Mtendaji Mkuu wa TLS,  Emilia Siwingwa.
         Akizungumza na Waandishi wa habari, Rais wa Chama hicho, amesema, kwa ujumbla muswada ni mzuri kutokana na maudhui yake, lakini una kasoro nyingi ambazo ikiwemo kuwanyima wananchi wengi kushiriki katika kutoa maoni.
         Alisema, hatua ya muswada huo kupelekwa bungeni kwa hati ya dharura, kunasababisha muswada huo kujadiliwa na makundi machache ya wananchi kama ambavyo sasa maoni yanafanyika Dar es Salaam, Dodoma na Zanzibar badala ya kuwa nchi nzima.
     Stola  amesema, kutokana na kasoro ambazo TLS imebaini itakwenda kwa Rais Jakaya Kikwete kujaribu kumshauri mambo kadhaa na mapendekezo yao ikiwemo kuondoa hati ya dharura.

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช