.

TP MAZEMBE WATUA DAR

Apr 1, 2011

Timu ya TP Mazemba ya Jamhuri ya Kidemokrasi-DRC, imewasili leo jioni jijini Dar es Salaam, tayari kwa mtanange wao unaotarajiwa kuwa mkali dhidi yao na Simba ya hapa, kwenye Uwanja wa Taifa jijini, Jumapili hii. Kikosi va viongozi wa timu hiyo waliwasili mida ya saa 12 jioni kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere. Mechi hiyo ya ligi ya mabingwa Afrika. Habari inatarajiwa kuwa na mvuto wa aina yake kwa mashabiki kwa kuwa  Simba inahitaji kushinda mabao 2-0, kwani katika mechi ya awali iliyopigwa Lubumbashi Machi 20, Simba ilikwanyuliwa mabao 3-1.

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช