Msafara wa timu hiyo utakuwa na jumla ya watu 29, wakiwemo wachezaji 21 na benchi la ufundi lenye watu sitaukiongozwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar(ZFA), Hafidh Ally Tahir.
Wachezaji watakaokuwemo katika msafara huo niShaaban Kado, Juma Abdul, David Luhende, Babu Ally, Shomari Kapombe, Jabir Aziz, Salum Aboubakar, Thomas Ulimwengu, Mbwana Samata, Kigi Makasi, Gharib Mussa, Mbwana Bakari, Idrisa
Abdulrahim, Innocent Wambura, Khamis Mcha, Awadh Issa, Amour Suleiman, Himid Mao, Mrisho Ngassa na Salum Telela.
Aprili 13 mwaka huu timu hiyo ilikabidhiwa jumla ya sh. milioni2 2 ambazo iliahidiwa endapo ingeitoa Cameroon kwenye michuano ya Olimpiki. Fedha hizo ziliahidiwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) na kampuni ya
Simba Trailers.
NSSF kupitia kwa Mkurugenzi Mkuu wake Dk. Ramadhan Dau ilikabidhi sh. milioni 10, wakati Azim Dewji ambaye ni Mkurugenzi wa Simba Trailers alikabidhi sh. milioni 12.
Kati ya fedha hizo ilizotoa Simba Trailers, sh. milioni 10 ni kwa ajili ya timu, sh. milioni 2 kwa ajili ya kipa aliyeokoa penalti na wafungaji wa
mabao mawili ya U23.
U23 imepangiwa kucheza na Nigeria katika raundi ya pili ya michuano ya Olimpiki ambapo mechi ya kwanza itachezwa jijini Dar es Salaam kati ya Juni 4 na 5 mwaka.
Picha zaidi za kuagwa timu hiyo.
Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Kanali Mstaafu, Iddi Kipingu akiwapiga msasa wachezaji wa timu hiyo. Kushoto ni Rais wa TFF, Leodegar Tenga.
Nahodha wa timu hiyo Shabani Kado akiahidi ushindi kwa timu hiyo.
Kocha Jamhuri Kihwelo 'Julio' yeye akasema hawataki sifa kwa sasa, sifa itakuja baadaye.
Wachezaji wa timu hiyo waliondoka leo kwenda Uganda.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269