.

YALIYOJIRI TAMASHA LA PASAKA DIAMOND

Apr 25, 2011

  KICHEKO CHA 'MENO  THELATHINI NJE' KWA  RAIS!
  MBUNGE wa Rombo kwa tiketi ya CHADEMA, Joseph Selasini  akimsalimia Rais Jakaya Kikwete kwa furaha ya aina yake, wakati alipokutana na Rais, kwenye Tamasha la wasanii wa nyimbo za injili lililofanyika Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam jana.
SHIKAMOO YA WATOTO
Mtoto ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja akimsalimia Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete muda mfupi baadaya kuwasili katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam ambapo alikuwa mgeni rasmi katika tamasha la wasanii wa nyimbo za dini lililofanyika jana.
UZINDUZI
Rais Dkt Jakaya Mrisho kikwete akizindua album ya Haleluya collection yenye nyimbo za wasanii mbalimbali wa injili wakati wa tamasha la wasanii wa nyimbo za dini lililofanyika katik ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salam jana mchana.Katikati ni mratibu wa Tamsha hilo Bwana Alex Msama na kulia ni Askofu Samson Kameta(Picha  zote na Freddy Maro).

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ª