Breaking News

Your Ad Spot

May 18, 2011

MWENYEKITI MWANZILISHI WA CCJ RICHARD KIABO AKANUSHA NAPE, MWAKYEMBE, SITTA NA MWAMBALASWA KUWA WAANZILISHI WA CHAMA HICHO KAMA INAVYODAIWA NA CHADEMA

TAARIFA KAMILI BILA YA NYONGEZA HII HAPA

Mweneyekiti mwanzilishi wa Chama Cha Jamii (CCJ)
Richard  Kiabo akizungumza na Waandishi wa habari
mjini Dar es Salaam, leo. Kulia ni Katibu wa CCM mkoa
wa Dar es Salaam, Kilumbe Ng'enda.


Kutokana na uvumi na matamko mbalimbali kutoka kwa wanachama na baadhi ya wasemaji wa Chadema juu ya waanzilishi wa CCJ. Mimi niliyekuwa Mwenyekiti na mwanzilishi wa CCJ Taifa, napenda kufafanua kama ifuatavyo  kuweka wazi jinsi na namna mbalimbali ilivyoabzishwa CCJ, pamoja na wale waliohusika hasa, tofauti na onavyotaka kupotoshwa.                     
A. KUANZIOSHWA  KWA CCJ         
Kirefu cha CCJ ni Chama Cha Jamii ambacho kilianzishwa na baadhi ya wananchi wa Tanzania. Chana hiki kilipata rasmi usajili wake wa muda, Machi 2, 2010.
Viongozi waanzilishi walikuwa ni:-
1. Ndugu Richard A. Kiyabo- Mwenyekiti Taifa
2. Ndugu Renatus Muabhi- Katibu Mkuu.
Kutokana na taratibu za usajili wa vyama vya siasa hapa nchini ilibidi tuanze harakati za kutafuta wanachama, tunashukuru kwamba Watanzania wengi walituunga mkono na hata kujiunga na chama chetu, na hatimaye kufikia kupata usajili wa muda, na miongoni mwa watu waliojiunga na chama chetu ni pamoja na Mh. Frederick Mpendazoe.
Mpendazoe alitaka awe Mwenyekiti wetu wa Taifa lakini hatukukubali ombi lake ambalo hakuliwakilisha kimaandishi bali kwa mdomo tu, lakini aliapishwa na chama kuwa msemaji wa CCJ.
Waheshimiwa ambao Mpendazoe anadai walikuwa waanzilishi wa CCJ, hoja hiyo ni ya utata mkubwa maana CCJ haikuwahi kuwa na waanzilishi wa aina hiyo yaani:-
1. Mh. Nape Nnauye
2. Mh. Harison Mwakyembe
3. Mh. Samwel Sitta na
4. Mh. Ezekiel Mwabalaswa
Swali la kumuuliza Mh. Mpendazoe ni je alipotangaza kutoka CCM waliompokea CCJ walikuwa hao aliowataja? na je wao walikuwa na nyadhifa zipi na kadi namba ngapi za uanachama? Je amesahau kuwa alinukuliwa na vyombo vya habari akimkaribisha Mh. Sitta kwamba ajiunge na CCJ? hilo atasemaje? Someni gazeti la Mwanachi, ISSN 0856-7573 Namba 03580 la April 6, 2010.
Napenda kuwakumbusha wanasiasa hasa wa Chadema kwamba siasa za udaku hazitawafikisha Ikulu, Watanzania ni waelewa na wala siyo mbumbumbu kama ambavyo Chadema wanajaribu kuonyesha.
Nawakumbusha kwamba Watanzania wamekua kisiasa ndiyo maana hawakuwaingiza IkuluChadema kwa kura zao. Kupigiwa makofi kwenye mikutano ya hadhara siyo kupewa kura kwenye chumba cha kupiga kura, Watanzania wanaelewa kwamba akili za kuambiwa kwenye mkutano changanya na zako kwenye chumba cha kupiga kura.
Nawashauri Mpendazoe na wenzake wa Chadema waache siasa za udaku, Watanzania wanataka kusikia sera za chama husika si udaku.
Wakiendelea na udaku wa kuwatuhumu watu kila kukicha mwisho tutaanza kuamini kwamba pengine hiyo ndiyo sera ya chama chao isiyo rasmi kimaandishi
Kama hawana la maana la kuwaambia wananchi ni bora wakanyamaza kuliko kuwahutubia wananchi uzushi tu kila kukicha.
B. CHADEMA NA HARAKATI ZA PEOPLES POWER
Chadema wameonyesha kuwa nguvu ya umma si kura tena, bali maandamano na vurugu zenye lengo la kuitoa serikali madarakani. wao wanajiita Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, ajabu wanayotenda siyo ya kidemokrasia tena bali ni kuwa sasa Chama chao ni cha maandamano na vurugu.
Je Wanaiheshimu kweli Demokrasia? Wakumbuke kwamba serikali iliyopo madarakani iliwekwa na Watanzania kwa kura zao sasa kwa nini hawawaheshimu Watanzania?
Wasidhani kwamba demokrasia ya kweli nchini ni mpaka Chadema ishinde uchaguzi. La Hasha! Demokrasia ni pamoja na kuheshimu maamuzi ya wananchi kwa njia ya kura zao.
Huu ni wakati wa kujengaa taifa letu tukishirikiana na Serikali yetu, na si wakati wa vurugu, maandamano kila kukicha, Watanzania tuwe makini na Wanasiasa wasio utakia mema utaifa wetu na amani ya nchi yetu.
Tukumbuke kwamba suala na amani ni sawa na nyanya, nyanya ikitumbuliwa kuishona tena haiwezekani. bila amani shughuli za  kimaendeleo haziwezi kufanyika na hata shughuli zao wenyewe Chadema hawataweza kuzifanya.
Maisha ya wananchi kwa ujumla wake yanategemea amani katika nchi, hivyo sisi Watanzania hatuna budi kulipa kipaumbele suala la amani na maendeleo ya nchi yetu. Maneno yetu wanasiasa yawe ya kujenga na wala si ya kubomoa amani yetu, na tujifunze kuwa wakweli badala ya kuendekeza siasa za udaku.
MUNGU IBARIKI AFRIKA, MUNGU IBARIKI TANZANIA
Richard A, Kiabo
Kada wa Chama Cha Mapinduzi

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages