Breaking News

Your Ad Spot

May 29, 2011

WANAHARAMU WAMTIA UMASIKINI MWAIKENDA; WAMPORA KAMERA, LAP TOP NA VITENDEA KAZI KIBAO

Na Mwandishi Wetu

MPIGAPICHA Mkuu wa gazeti la Jambo Leo, ambaye pia ni Mmiliki wa Blogu ya Kamanda wa Matukio, Richard Mwaikenda ameporwa begi lenye kamera na kompyuta na
vibaka waendesha pikipiki.

Vibaka hao waliokuwa wamepakizana kwenye pikipiki, walimpora begi hilo lililokuwa kiti cha mbele cha gari lake alilokuwa akiendesha, likiwa karibu na makutano ya barabara za  Kitunda na Nyerere, eneo la Banana, Ukonga, Dar es Salaam Jumamosi wiki iliyopita.

Aliyechukua begi kwenye gari ni kibaka aliyepakizwa nyuma na pikipiki hiyo kuondoka kwa kasi kuelekea
Ukonga na kumwia vigumu mpiga picha huyo kuachia usukani kuwafukuza kwani magari yalikuwa yameanza kutembea.

Alitaja vitu vingine vilivyokuwemo kwenye begi hilo kuwa ni, Modemu ya Vodacom, kifaa cha kutolea picha kutoka kamera ya digital kwenda katika kompyuta (Card reader),
Flash, vitambulisho vya kazi na nyaraka muhimu.

Akisimulia tukio hilo, Mwaikenda alisema , inaelekea vibaka hao walimfuatilia kutoka Kitunda ambapo
alisimamisha gari lake na  kuchukua kamera kwenye begi na kupiga picha mashimo makubwa barabarani karibu na Kituo Kidogo cha Polisi cha Kitunda.

Mwaikenda alikuwa anatokea nyumbani kwake, Kivule kwenda Pugu Kanisani  kuripoti tukio la Ibada ya misa ya shukrani kwa Hayati Papa John Paul wa Pili kutangazwa Mwenye Heri.

Nkoromo Daily Blog, inatumia fursa hii kumpa pole Kamanda wa Matukio. ikiamini kwamba za mwizi arobaini

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages