Breaking News

Your Ad Spot

Jun 27, 2011

NAPE ALIVYOTIKISA LINDI MJINI

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye akimkabidhi kabrasha la kuorodhesha wanachama, Mwenyekiti wa CCM Kata ya Mtanda, wilaya ya Lindi Mjini, Issa Malocho,alipofanya mkutano wa wajumbe wa mashina, leo katika ukumbi wa oceanic View, mjini Lindi. Jumla ya Kata 18 zilipewa fomu hizo kwa ajili ya kuorodhesha wanachama wa CCM katika maeneo yao. 
Wajumbe wa mashina kutoka kata 18 za Wilaya ya Lindi mjini, wakiwa katika mkutano wao na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye  kwenye ukumbi wa Ocenic View mjini Lindi. 
Nape akisakata muziki na vijana wa kikundi cha sanaa cha mjini Lindi katika mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika leo, kwenye uwanja wa Fisi mjini Lindi. 
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye akihutubia umati wa watu katika mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya Uwanja wa Fisi mjini Lindi leo. 
Katibu wa NEC, Oganaizesheni CCM, Asha Abdallah Juma akihutubia umati wa watu katika mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya Uwanja wa Fisi mjini Lindi leo. 
Nape akisisitiza jambo wakati akihutubia kwenye mkutano huo kwenye uwanja wa fisi 
Mmoja kati ya wananchi waliohudhuria mkutano wa hadhara wa CCM kwenye Uwanja wa Fisi mjini Lindi akifurahia hotuba. 
Wananchi wakishangilia wakati wa mkutano wa hadhara wa CCM kwenye Uwanja wa Fisi mjini Lindi leo. 
Nape na Asha Abdaallah Juma wakiaga wananchi baada ya mkutano huo

1 comment:

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages