Breaking News

Your Ad Spot

Jun 28, 2011

NAPE AMALIZA ZIARA LINDI SASA YUPO MTWARA

KATIBU wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimjulia hali Somoye Ismaili (70) aliyekuwa akisubiri matibabu kwenye chumba maalum cha kuhudumia wazee, katika hospitali ya Wilaya ya Lindi mjini, juzi. Nape alitembelea hospitali hiyo, mwishoni kwa ziara yake ya siku mbili mkoani Lindi. Wapili kulia ni Katibu wa NEC, Oganaizesheni CCM, Asha Abdallah juma. 
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Lindi Ali Mtopa (kushoto) akiuaga msafara wa Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, wakati msafara huo ulipokuwa tayari kuingia mkoani Mtwara kuendelea na ziara yake Juni 27, 2011. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mtwara, Alhaji Dadi Mbulu. 
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akizungumza na wananchi wa wilaya ya Newala mkoani Mtwara walipoupokea msafara wake akiwa njiani kwenda Mjini Liwale. Juni 27, 2011 
Katibu wa NEC, Oganaizesheni, Asha Abdallah Juma akizungumza na wananchi wa wilaya ya Newala mkoani Mtwara walipoupokea msafara wake na Nape, wakiwa njiani kwenda Mjini Liwale. Juni 27, 2011 
Wasanii wa kikundi cha hamasa cha Newala mkoani Mtwara wakitumbuiza baada ya kupokea msafara wa Katibu Nape ulipokuwa njiani kwenda Mjini Liwale. Juni 27, 2011 
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akishiriki kucheza ngoma ya kikundi cha uhamasihaji cha vijana wa Newala, baada ya msafara wake kuwasili mjini Newala, Juni 27, 2011 
Katibu wa Oganaizesheni CCM, Asha Abdallah Juma (kushoto) akishiriki kucheza ngoma ya kikundi cha uhamasihaji cha vijana wa Newala, baada ya msafara wake na Nape kuwasili mjini Newala, Juni 27, 2011
Nape akisalimia wazee wa Newala alipokwenda kufanya mkutano wa ndani na  viongozi wa mashina na wajumbe wa nyumba kumi wa CCM kwenye ukumbi wa Chama Cha Akiba na Mikopo (SACCOS) mjini Newala mkoani Mtwara. Juni 27.
Viongozi wa mashina na wajumbe wa nyumba kumi wa CCM wakiwa kwenye mkutano wao wa ndani na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, kwenye ukumbi wa Chama Cha Akiba na Mikopo (SACCOS) mjini Newala mkoani Mtwara. Juni 27. 
Nape akicharaza ngoma baada ya kuwasili katika Tandahimba mkoani Mtwara kwa ajili ya mkutano wa hadhara, Juni 27. 
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akipokea kadi kutoka kwa aliyekuwa mwanachama wa CUF, Rukia Panyota, aliyeamua kurejea CCM wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika wilayani Tandahimba mkoani Mtwara. Juni27. 
Mashabiki wa CCM wakishangilia wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika wilayani Tandahimba mkoani Mtwara, Juni 27.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages