Breaking News

Your Ad Spot

Jun 7, 2011

SIMBA NA YANGA KUVAANA LEO UWANJA WA SAMORA

Na Mwandishi Wetu
TIMU ya Simba na Yanga All Star leo zitacheza mechi ya kirafiki itakayofanyika kwenye Uwanja wa Samora uliopo Mjini Iringa.

Akizungumza na gazeti ili jana mratibu wa pambano hilo la watani wa jadi Ally Mduba, alisema kuwa pambano hilo ni maalum kwa wakazi wa Iringa ambao hawajawahi kuona watani hao wa jadi
wakichuana.

Mduba alisema wameamua kuzipeleka timu hizo mkoani humo ili kutoa nafasi kwa wakazi wa Iringa kushuhudia wachezaji hao ambao waliwahi kuvuma katika miaka ya 90.

Alisema mchezo huo utaanza  saa 10:30 jioni na yote yamekamilika. Vikosi vya timu hizo vimeshawasili mkoani humo kwa ajili ya mchezo huo.

Kikosi cha Yanga kinaundwa na Kipa Peter Manyika, Bakari Malima, Edibily Lunyamila, Idd Moshi,
Salvatory Edward, Omary Kapilima, Ephrahim Makoye, Ben Mwalala na Ally Yusuph Tigana.
Kikosi cha Simba kina wachezaji Issa Manofu, Thomas Kipese, Boniface Pawasa, Madaraka
Suleiman, Shekhan Rashid, Edwin Mukenya, Suleiman Matola, Yusuph Macho, na Said Swed

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages