Na Andrew Chale
HARAMBEE iliyokuwa ifanyike kesho Julai 8 ya kuchangisha Euro 127,058 za vifaa vya hospitali za Rufaa nchini iliyoandaliwa na Taasisia ya ALLURE International kwa kushirikiana na Wizara ya Afya imehairishwa mpaka hapo baadae itakapotangazwa tena.
Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo katika Hoteli ya Moven Pick jijini Dar salaam, Mkurugenzi wa Allure International, Jacqueline Haidery alisema kuwa wamesogeza mbele kwa sababu zilizonje ya uwezo wao ikiwemo majukumu mbalimbali walizokuwa nazo wageni maalum ambao ni viongozi wa Serikali walikuwa wafike kwenye shughuli hiyo hiyo kesho.
“Harembee maalum ya kuchangia vifaa vya hospitali za rufaa na za mikoa kiasi cha Euro 127,058 ambazo tulikuwa tuzifanye Julai 8,(kesho) kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu na wenzetu wa wizara ya afya, tumeahirisha mpaka hapo baadae hivyo tunaomba radhi kwa usumbufu kwa wageni na wadau waliochangia kadi maalum za harembee hiyo” alisema Jacqueline.
Allure na Wizara ya Afya waliandaa harembee hiyo maalum ambayo ilikuwa ifanyike leo Moven pick, jijini Dar es Salaam, kwa kukusanya kiasi hicho cha Euro 127,058 ambazo zitaenda kununulia vifaa kwenye Hospitali za Rufaa za Mbeya na Bugando sambamba na zile za mikoa ya Kaskazini na kusini ilikukabiliana na upungufu huo.
Aidha Jacqueline Haidery alisema kuwa kwa wageni wanaweza kuwasilina kupitia anuani za Allure zilizopo kwenye kadi maalum.
Your Ad Spot
Jul 7, 2011
Home
Unlabelled
ALLURE INTERNATIONAL YASOGEZA MBELELA HAFLA YA UCHANGISHAJI EURO 127,058, ILIYOKUWA IFANYIKE KESHO
ALLURE INTERNATIONAL YASOGEZA MBELELA HAFLA YA UCHANGISHAJI EURO 127,058, ILIYOKUWA IFANYIKE KESHO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269