Breaking News

Your Ad Spot

Jul 7, 2011

PPAT YALAANI WAANDISHI WA HABARI KUSHAMBULIWA DAR

KUMB.Na:GS/PPAT/01/2011 7 Julai ,2011
MHARIRI WA HABARI
………………………………
YAH: TAMKO LA PPAT KULAANI KUSHAMBULIWA KWA MPIGAPICHA HERI SHABANI WA GAZETI LA MAJIRA NA MWANDISHI CHRISTOPHER LISA WA SANI

Chama cha Wapigapicha za Habari Tanzania (PPAT) kinapenda kuungana na watanzania
wote kulaani kitendo cha Kinyama alichofanyiwa Mpigapicha wa Gazeti la Majira na
Mwandishi wa Sani, kwa kuvamiwa na wananchi, kupigwa na kuporwa mali zao wakati
wakiwa kazini kuripoti tukio la vurugu za kundi la vijana waliokuwa wakishambulia polisi
kwa mawe baada ya Polisi kuchukua Mwili wa Marehemu Bakari Hamisi ambaye ndugu zake
waligoma kuu zika Julai 6, 2011.
Kitendo walicho fanyiwa Wanahabari hao ni cha Kinyama na katu hakiwezi kuvu milika.
Hivyo tunaliomba Jeshi la Polisi lifanye kazi yake ipasavyo na kuhakikisha wote waliofanya
vurugu hizo wanapatikana na kufunguliwa mashitaka kwa vitendo hivyo vya vurugu na
kujeruhi watu na kuharibu mali.
Kumekuwapo na vitendo vingi vya kinyama wanavyofanyiwa Waandishi wa Habarui hasa
Wapigapicha kwa kupigwa na wananchi ama Polisi ambao kimsingi wanajua kazi na wajibu
wa Wanahabari katika jamii.
Pia hivi karibuni, katika Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea
Mpigapicha wa Mwananchi Communication Fidelis Felix akiwa kazini alishambuliwa na
kuharibiwa Camera yake na Askari.
PPAT inapenda kuliomba Jeshi la Polisi kutoa elimu kwa Askari wake kuwa Mwandishi wa
Habari si mtu wa kubugudhiwa na kupigwa wakati wanafanya kazi zao kwani kufanya hivyo
ni kuinyima haki jamii kupata habari mbalimbali zinazo tokea katika jamii.
PPAT inawapa pole Heri Shabani na Christopher Lissa kwa mswaibu yaliyowafika na Mungu
awape nguvu na kurejea tena katika kazi.
Mroki Mroki
Katibu Mtendaji PPAT.
0717002303/0755 373999

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages