WABUNGE WAIKATAA BAJETI YA NGELEJA, PINDA AOMBA WIKI TATU IKARABATIWE KABLA YA KUSOMWA TENA BUNGENI, BARUA YA JAIRO YAZUA KASHEHE, YAMUWEKA MATATANI!
Bajeti ya Wizara ya Nishati ya Madini iliyowasilishwa na Waziri wa wizara hiyo, William Mganga Ngeleja leo Bungeni mjini Dodoma, imetupiliwa mbali na Wabunge na kusababisha Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuomba serikali ipewe wiki tatu ili iweze kuirekebisha abajeti hiyo kabla ya kuirudisha isomwe upya bungeni.
Ngeleja |
Kufuatia hatua hiyo, Spika wa Bunge anne Makinda ameafiki kukataliwa bajeti hiyo akisema ni nyeti na kutaka itakaporejeshwa atena bungeni iwe na majibu yanayotosheleza maswali yaliyopo na uhalisia na mipango ianayotekelezeka kwa kuzingatia athari ambazo wananchi na nchi yenyewe kwa jumla inazopata kutokana na ukosefu wa umeme uliokithiri. Ingawa baada ya bunge kuahirishwa Waziri Ngeleja ameonyesha kwamba ni jambo muhimu bajeti yake kukataliwa akisema ilitengewa fedha kidogo kulingana na mikakati na mipango yake, lakini huenda ikamuweka bapaya yeye na Katibu Mkuu wa wizara hiyo David Jairo (ambaye pamoja na bajeti kuonyesha kutokidhi mahitaji pia barua aliyoziandikia taasisi zilizopo chini ya Wizara hiyo zitoe mchango wa sh. milioni 50, ili kufaikisha mchakato wa kusomwa bajeti hiyo bungeni kama barua hiyo inavyosomeka hapo.
Jairo |
ngeleja umefulia achia ngazi
ReplyDelete