Breaking News

Your Ad Spot

Jul 5, 2011

FISH GROUP WASAKA WADHAMINI

Na Andrew Chale
KUNDI la sanaa za maigizo na filamu la Fish
Group Filam linasaka wadhamini ilikuendelea
kukuza vipaji vya wasanii wachanga na kuinua
tasnia ya filamu nchini.

Wakiongea na mwanahabari mapema leo 
ofisini kwao Magomeni jijini Dar es Salaam,
jana viongozi wa kundi Hamis Yusuph na Juma
Mwamwindi ‘Stopa’ walisema kuwa wanasaka
wadhamini hao kwa kuwa mpaka sasa tayari
wamesha wandaa vijana kwa kiwango
kikubwa kwenye sanaa huku wengine
wameokolewa kwenye makundi  mabaya na
kuwaweka pamoja.

“Lengo letu kukuza vipaji na kuendeleza sanaa
hivyo tunaomba wadau kujitokeza na kutupa
tafu ya kuendeleza gurudumu hili mpaka sasa
tunajiendesha wenyewe bila wadhamini”
alisema Mwamwindi ‘Stopa’.

Mpaka sasa kundi hilo linawasanii 64 na
linanolewa na walimu wazoefu wakiwemo
Hamad Abdala ‘Mr.Eddo na Mode ambao ni
wasanii wazoefu kwenye tasnia hiyo.

Aidha waliongeza kuwa, malengo yao zaidi ni
kuakikisha mbaali na sanaa ya maigizo na
filamu pia wanataka kuwa na kundi la ngoma
na sarakasi.

Kwa upande wake mkuu wa nidhamu wa kundi
hilo, Ramadhan Shaban ‘Max well’ alisema
kuwa wamepata faraja kwa wazazi wa
wasanii waliojiunga na kundi hilo kuwaunga
mkono kwa kuwaruhusu watoto wao kufanyaa
sanaa tofauti na zamani ambapo sanaa
ilionekana kama uhuni. “Tunajisikia faraja
wazazi kuikubali sanaa hivyo Tanzania
tunakoelekea soko litakuwa zaidi ni
kushirikiana kwa pamoja” alisema Max.

........
 unaweza wasiliana nao kupitia anuani
zifuatazo;0652513951 AU 0719302000  ama
unaweza kufika ofisini kwao Magomeni Mapipa
,kituo cha mabasi cha Mapipa mkabala na
Shibam Restaurant.
 Kiongozi wa kundi hilo, Juma Mwamwindi ‘Stopa’  akiwa na baadhi ya wasanii wa wanaounda kundi la Fish Gruop Filamu, la Magomeni jijini Dar es Salaam
      Baadhi ya wasanii hao wakiwa kwenye picha ya pozi

1 comment:

  1. Jamani wasaidieni hawa, huenda tukapata waigiizaji bora, tusiangalie majina ya waigizaji wakubwa tu, tujue kuwa avumaye papa baharini, lakini samaki wengine wapo!

    ReplyDelete

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages