NA MWANDISHI WETU
KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL), kupitia bia yake ya Kilimanjaro Premium Lager imezindua kampeni ya 'Jivunie Utanzania' kuunga mkono maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania.
Uzinduzi wa kampeni hiyo uliofanyika leo kwa shamrashamra za ina yake kwenye viwanja vya akumbusho ya Taifa mjini Dar es Salaam, na kuhudhuriwa na viongozi wa ngazi za juu wa TBL na wageni wakiwemo baadhi ya watu walioipatia sifa nchi katika medani mbalimbali ikiwemo michezo.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa TBL, Robin Goetzsche, alisema, wakati esemba tisa mwaka huu itatimia miaka 50 tangu Tanzania ipate uhuru wake, Kilimanjaro Premium Lager tasherehekea mafanikio hayo muhimu kupitia kampeni hiyo ya 'Jivunie Utanzania".
Alisema, bia hiyo ambayo imepewa jina la Kilimanjaro Premium Lager kutokana na jina mlima Kilimanjaro ambao ni mrefu zaidi barani Afrika uliopo Tanzania, itatumia kampeni hiyo kuwakumbusha Watanzania walikotoka na kule wanakokwenda.
"Tutatkuwa tunasherehekea juu ya umbali tuliotoka, kama watu na kujikumbusha sote kwamba japokuwa mambo si makamilifu, bado kuna sababau nyingi za kutufanya kujivuna badala ya kupuuza", alisema Mkurugenzi huyo.
"Muhimu zaidi Kilimanjaro Premium Lager inalenga kutushawishi kuendeleza jitihada ili kupata mafanikio makubwa zaidi ili katika miaka 50 ijayo tuendelee kusherehekea maendeleo yetu", aliongeza.
Naye Mkurugenzi wa Masoko wa TBL, David Minja, alisema kampeni hiyo itakuwa ikishereheshwa kwa matukio mbalimbali kuanzia mwezi huu (Julai 2011) hadi Desemba 2011 siku ya kilele cha maadhimisho siku Uhuru.
Alisema, mwishoni mwa kampeni hiyo kutakuwa na mbio za kuipeperusha bendera ya Taifa zikijumuisha mikoa minne ambayo hakuitaja, na kwamba mbio hizo ambazo kila mkimbiaji atakuwa na kitambaa chenye rangi moja kati ya zile nne za bendera ya taifa, zitamalizikia kwenye lango la Mweka, Moshi mkoani Kilimanjaro.
Minja alisema baada ya wanariashara hao kukutana vitambaa hivyo viyaungwa na kuwa bendera moja ya taifa ambayo itapelekwa kusimikwa kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro kama alivyofanya Luteni mstaafu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Alexander Nyirenda kwa bendera ya Tanganyika na Mwenge wa Uhuru kwenye kilele hicho miaka 50 iliyopita.
Alitaja mambo sita yatakayonadiwa kuwakumbusha Watanzania katika kampeni hiyo ya 'Jivunie Utanzania' kuwa ni umuhimu wa Watanzania kuenzi amani na utulivu, Kiswahili, heshima na ukarimu walio nao Watanzania.
Your Ad Spot
Jul 5, 2011
Home
Unlabelled
TBL YAZINDUA KAMPENI YA'JIVUNIE UTANZANIA' KUUNGA MKONO MAADHIMISHO YA
TBL YAZINDUA KAMPENI YA'JIVUNIE UTANZANIA' KUUNGA MKONO MAADHIMISHO YA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269