Breaking News

Your Ad Spot

Jul 17, 2011

VODACOM FOUNDATION SERENGETI WILD DOG PROJECT

Waziri wa wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige akijadiliana kuhusiana na masuala ya uhifadhi na utalii na mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Vodacom Tanzania Dietlof Mare,kabla ya uzinduzi rasmi wa mradi wa (Vodacom Foundation Serengeti Wild Dogs Conservation Project) Kulia ni mjumbe wa bodi ya wadhamini ya Vodafone Foundation toka nchini Uingereza, Bi Elizabeth Filkin. 
Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania  Dietlof Mare akimkabidhi sanamu ya mbwa mwitu Mkurugenzi wa shirika la Hifadhi za Taifa TANAPA Allan Kijazi kama ishara ya uzinduzi rasmi wa mradi wa utunzwaji wa mbwa mwitu katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti (Vodacom Foundation’s Serengeti Wild Dogs Conservation Project). Mradi huo ulizinduliwa juzi na Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige (katikati) ambapo Vodacom Foundation imetoa dola za Kimarekani 450,000 kwa miaka mitatu. 
Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania Dietlof Mare, wakifurahia jambo na Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige, baada ya kuwasili kwenye kambi ya utalii ya Soroi, Serengeti kwa ajili ya uzinduzi wa mradi wa kuhifadhi mbwa mwitu (Vodacom Foundation’s Serengeti Wild Dogs Conservation Project) katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige akiwa anakabidhiwa sanamu ya mfano wa mbwa mwitu na Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania, Dietlof Mare, mara baada ya kuzindua mradi wa uhifadhi mbwa mwitu katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti mradi ambao unafadhiliwa na Vodacom Foundation kwa dola 450,000 kwa miaka mitatu.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages