Breaking News

Your Ad Spot

Aug 7, 2011

CHADEMA KWATIFUKA, KAMATI KUU YAWAFUKUZA UANACHAMA MADIWANI WATANO WA RUSHA

Madiwani hao niMadiwani waliofukuzwa uanachama ni Estomiah Mallah, John Bayo, Charles Mpanda, Rehema Mohammed na Reuben Ngowi.
Kwa mujibu wa Mbowe, madiwani hao pamoja na wengime watano waliotii maelekezo ya kamati kuu, walitakiwa kutekeleza maagizo ya kamati hiyo iliyoyatoa katika mkutano wake wa Julai 17, mwaka huu.
Alisema maelekezo hayo yalikuwa yanawataka madiwani hao kujiuzulu nafasi walizopata pamoja na kuomba radhi kwa makosa waliyoyapata kutokana na mwafaka uliofikiwa na madiwani wenzao wa TLP na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Mbowe alisema, kimsingi, chama hicho hakikuridhika wala kutambua kuhusiana na mwafaka huo, ambao uliishia kwa madiwani hao wa CHADEMA kupatiwa vyeo, ikiwemo nafasi ya naibu meya wa Halmashauri ya Jiji la Arusha na kamati nyingine za halmashauri hiyo.
Habari zilizopatikana kutoka Dodoma zimedai kwamba Madiwani hao wamefukuzwa saa sita usiku, baada ya kuitunishia misuli Kamati Kuu ya CHADEMA kwa kukataa kuhojiwa mmoja baada ya mwingine na badala yake wakataka wahojiwe kwa pamoja, la sivyo liwalo na liwe.


Wamefukuzwa kwa kuonekana wamekula dili na CCM na kukubali mwafaka hali ambayo uonfozi wa Chadema uliwashushia tuhuma madiwake wake hao kwamba wamelamba rushwa inagwa wenyewe walikana vikali na kuomba ushahidi kuthibirisha hilo.


Madiwani hao mwanzoni mwa sakata hilo, walisema wameamua kuingia mwafaka na CCM kwa sababu ya uchu wao wa kutaka maendeleo zaidi katika jiji la Arusha badala ya mitafaruku inayochelesha maendeleo.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages