Breaking News

Your Ad Spot

Aug 9, 2011

TAMASHA LA SIMBA LAFANA A-TOWN, MASHABIKI KIBAO WAJITOKEZA

KIKOSI CHA SIMBA
Tamasha la klabu ya Simba linalofanyika kila mwaka lililofanyika leo jijini Arusha limefana baada ya mashabiki wengi wa klabu hiyo kutoka mikoa ya kanda ya kaskazini kujitokeza kwa wingi na wengine wapya kujiunga na klabu hiyo.

Katika jukwaa maalumu lililoandaliwa kwaajili ya kuwapatia wanachama wapya kadi za uanachama walionekana mashabiki wengi wakichukua kadi zao za uanachama pamoja na kujiorodhesha ambapo hadi mchezo unakamilika taarifa zilieleza kuwa ni zaidi ya mashabiki 120 waliojiunga.

Tamasha hilo lililofanyika katika uwanja wa kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid limeonekana kufana kutokana na majukwaa yote kufurika watu hadi kukosekana kwa nafasi za watu kuendelea kuingia uwanjani hapo.

Hata hivyo tamasha hilo lilitawaliwa na kejeli mbalimbali ikiwemo baadhi ya watu wanaoaminiwa kuwa mashabiki wa klabu ya Yanga walioingia uwanjani hapo wakiwa wamevalia sare za Yanga hali ambayo ilisababisha mashabiki wa Simba kuwatoa uwanjani.

Tamasha hilo lililopambwa na burudani mbalimbali ikiwemo pambano la soka la utangulizi lililoikutanisha timu ya soka ya makocha Arusha na viongozi wa Simba Dar es salaam ambapo timu ya viongozi wa simba ilishinda kwa magoli 2-1.

Katika mchezo huo timu ya makocha Arusha ilitangulia kupata bao katika dakika ya 4 kupitia kwa Mohamed Laizer kwa shuti kali lililomshinda mlinda mlango maarufu nchini Idd Pazi.

Goli la la kusawazisha la simba lilipatikana katika dakika ya 22 ya mchezo kupitia kwa Swed Mkwabi ambae ni mjumbe wa kamati ya utendaji ya Simba kwa shuti kali na dakika ya 71 timu ya viongozi wa Simba ilipata bao la pili kupitia kwa Salum Kambaya baada ya kuwaacha kwa kasi walinzi wa timu ya makocha.

Katika mpambano huo uliwakumbusha mbali mashabiki wa soka mkoani Arusha kutokana na kuwaona waakongwe wa soka kama vile Godfrey Nyange Kaburu,Mosses Basena ambae ni kocha mkuu wa Simba,Richard Emetri ambae ni msaidizi wa kocha wa Simba,Ibrahim Masood ambae ni mjumbe wa kamati ya utendaji ya Simba,George Wakuganda,Said Tuli.

Kwa upande wa timu ya makocha Arusha walionekana wakongwe wa soka kama vile Rashid Idd Chama,Azizi Nyoni Njelambaya,Bakari Besti,Atuga Manyundo,Ramadhan Siwayombe na Imamu Abasi.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages