Breaking News

Your Ad Spot

Aug 22, 2011

TASWA YAIPONGEZA TIMU YA TAIFA YA GOFU YA WANAWAKE, KUTANGAZA JUMATANO KAMATI YA KUSIMAIA TAMASHA LA MICHEZO MIAKA 50 YA UHURU


Katibu Mkuu wa TASWA,
 Amir Mhando
 (A)      TIMU YA TAIFA YA GOFU WANAWAKE
CHAMA cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) kinatoa pongezi kwa timu ya Taifa ya gofu ya wanawake ya Tanzania ‘Tanzanite Stars’ ilitwaa ubingwa wa mashindano ya gofu ya Kombe la Challenge kwa wanawake katika nchi za Afrika Mashariki na Kati.
          Mashindano hayo yalianza Agosti 16 hadi Agosti 18, mwaka huu kwenye viwanja vya Klabu ya Gofu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Lugalo, Dar es Salaam.          TASWA imekunwa na mafanikio hayo na inatoa pongezi za dhati kwa timu hiyo kuweza kutetea ubingwa wake katika mashindano ambayo yanafanyika kila baada ya miaka miwili ambpo yalikuwa ya pili na ya viwanja 54.
      Tunasema vijana wetu wanastahili pongezi kwani nchi zote nne kutoka zilizoshiriki ambazo ni Kenya, Uganda, Zambia na wenyeji Tanzania zipo juu katika mchezo huo kwa wanawake. 
        Nchi za Rwanda, Burundi, Malawi, Ethiopia na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) zilishindwa kushiriki, lakini tatizo kubwa ni kukosa timu za wanawake.
       Tanzania ambao walikuwa mabingwa watetezi wa Kombe hilo ambalo kwa mara ya kwanza walitwaa mwaka 2009 Kampala, Uganda walitetea vema kwa kutwaa ubingwa kwa mara ya pili mfululizo.
Hayo ni mafanikio makubwa katika uongozi mpya wa Chama cha Gofu cha Wanawake Tanzania (TLGU) chini ya Rais, Mbonile Burton tangu kuingia madarakani Juni mwaka jana. Mafanikio haya yanafuatia yale ya kushika nafasi ya pili kwenye mashindano ya Afrika ya gofu kwa wanawake Abuja, Nigeria mwaka jana.
       Pia TLGU imeweza kutangaza vema gofu ya wanawake na kuweka historia ya kuandaa mashindano makubwa ya kimataifa kwa mara ya kwanza.
        Mwaka huu Tanzania wameibuka mabingwa kwa kishindo zaidi wakiwaacha wapinzani wao Zambia walioshika nafasi ya pili kwa tofauti ya mikwaju (strokes) 31. Mwaka 2009 ugenini walishinda kwa tofauti ya mikwaju 20.
        Tunaomba wachezaji wa Tanzanite Stars wakiongozwa na  nahodha Madina Iddi, Ayne Magombe, Angel Eaton na Hawa Wanyeche waone mafanikio haya waliyoyapata Watanzania wote tunayajali.
(B)  TAMASHA LA MICHEZO MIAKA 50 YA UHURU
Uongozi wa TASWA Jumatano Agosti 24, 2011 saa tano asubuhi utatangaza majina ya Kamati ya Kusimamia Tamasha la Michezo Miaka 50 ya Uhuru.
         Mkutano huo utafanyika hosteli za TFF Uwanja wa Karume, Dar es Salaam , hivyo ni imani yetu waandishi wengi watajitokeza. Pia tutazungumzia kuhusiana na semina mbalimbali ambazo chama kipo katika maandalizi ya kuzifanya.

Nawasilisha.

Amir Mhando
Katibu Mkuu TASWA

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages