Breaking News

Your Ad Spot

Sep 3, 2011

MAELEZO BINAFSI YA MGOMBEA WA CCM JIMBO LA IGUNGA DK. KAFUMU

DK. DALALY PETER KAFUMU (PICHANI)

FAMILIA
- Mke na Watoto Watano.

ELIMU
·         Shahada ya Uzamivu (Udaktari wa Falsafa - Ph.D) – Masuala ya Madini na Mazingira – 2000 Chuo cha Brussel, nchini Ubelgiji.
·         Shahada ya Uzamili  (MSc – Masuaa ya Madini na Mazingira) – 1995 chuo Kikuu cha Brussel, Nchini Ubelgiji na
·         Stashahada ya Uzamili (PG Dip – Masuala ya Utafutaji wa Madini) 1991 Chuo Kikuu cha Delft Nchini Uholanzi
·         Stashahada ya Uzamili (PG Dip – Masuala ya (Elimu)
1986 Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
·         Shahada ya Kwanza (BSc – Masuala ya Madini) – 1983
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

KAZI
-               Kamishna wa Madini, Wizara ya Nishati na Madini kuanzia mwaka 2006 hadi alipotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwa mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM.
-                
-               Mhadhiri wa nje wa Chuo Kikuu cha kilimo cha Sokoine (kuanzia mwaka 2005 hadi sasa.
-                
-               Mkurugenzi wa  Mawasiliano wa Wizara ya Nishati na Madini ambapo alikuwa mshauri na msemaji wa Wizara ya  Nishati na Madini ( 2004 – 206)
-                
-               Mkuu wa  Uhamasishaji wa Takwimu wa Idara ya Madini ambapo alihamasisha uwekezaji katika sekta nchini ili kukuza Uchumi  (2002 – 2004)
-                
-               Mtaalamu Mwandamizi wa Madini wa Wakala  wa Jiolojia Tanzania ambapo alifanya kazi ya kupima madhara matetemeko ya ardhi mafuriko na volcano na kushauri serikali hatua za kuchukua (1992 – 2002)

-               Makamu Mkuu wa Chuo cha Madini Dodoma ambako mafundi  sanifu wa  Sekta ya Madini  wamehitimu na wafanyakazi katika sekta (1988 – 1992)

-               Utafiti wa Madini katika maeneo ya Ziwa Victoria ambako kwa sasa  kimefunguliwa Migodi sita ya Dhahabu (1983 – 1998)


UJUMBE WA BODI
-               Bodi ya Usimamizi wa Makandarasi Nchini
-               Bodi ya Chuo Kikuu cha Dodoma
-               Bodi ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO).
-               Bodi ya Tasnia ya Uzinduaji (Uwazi katika Sekta ya Madini)
-               Bodi ya Mazingira ya Taasisi ya Sayansi na Teknolojia.

                     MCHANGO KATIKA MAENDELEO YA JAMII IGUNGA
-               Kuleta vitabu vya kiada na rejea katika Shule kumi za Sekondari (Itumba, Igunga, Mwamashimba, Mwisi, Nanga, Igurubi, Mwanzugi, Simbo, Choma, na Kininginila) .

-               Kujenga misikiti miwili kwa ajili ya wananchi wa Kata ya Itumba.

-               Akiwa Mwanachama wa Igunga SACCOS, amesaidia ushirika wa kifedha kwa kutoa Hisa, Ada na michango yake kwa wakati stahiki.

-               Kutoa Sh. milioni kumi na tano (15,000,000) kwenye Halmashauri kwa ajili ya ununuzi wa Madawati kwa shule za sekondari za Igunga.

-               Kuchangia ujenzi wa visima virefu vya maji vya Kata ya Itumba.
-               Nikiwa mlezi wa Vijana wa Igunga, nimewasaidia vijana wa Kata za Mwamashimba, na Itumba vifaa vya micezo ya mpira wa miguu (mpira, jezi na kombe), kuendesha ligi ya mpira wa miguu kwa vijana wa Kata ya Itumba

-               Kutoa mchango wa shilingi milioni moja (1,000,000) kwa ajili ya VICOBA kwa vijana wa Wilaya ya Igunga.

                   DIRA NA MWELEKEO WA UJENZI WA IGUNGA MPYA
-               Kuongeza kasi katika ujenzi wa miundombinu kama barabara, madaraja,  mabwawa na umeme vijijini.

-               Kuongeza na kupanua huduma za jamii vikiwamo, Elimu ya Msingi na Sekondari hususan kuwa na shule za sekondari zenye kidato cha sita; Zahanati na  Vituo vya Afya.

-               Kuweka pamoja nguvu za wananchi, wafadhili na  Serikali katika
kuekeleza azma hii ya kuleta maendeleo endelevu katika  Wilaya ya Igunga.

-               Kusimamia haki za wakulima na wafugaji   wanapouza mazao yao wapate bei yenye faida bila kupunjwa na kuwasaidia wachimbaji wadogo kushiriki katika shughuli za uchimbaji bila kusumbuliwa.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages