Breaking News

Your Ad Spot

Nov 4, 2011

MAHAFALI YA TANO YA CHUO KIKUU CHA TUMAINI, PJ WA CLOUDS FM, KWITEMA NA WADAU KIBAO WAPATA SHAHADA

 Wahitimu wa Shahada ya Sanaa ya Mawasiliano ya Umma ya Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira, Jeff Shelembi, Leonard Magomba, Emmanuel Kwitema na Paul James almaaruf PJ wa Clouds FM wakijadiliana jambo baada ya kutwishwa shahada zao katika mahafali ya chuo hicho yaliyofanyika leo kwenye viwanja vya Karimjee, Dar es Salaam.
 PJ akishukuru baada ya kukabidhiwa cheti chake katika mahafali hayo
 Doris Saivoiye akipokea cheti chake katika mahafali hayo
 Jeff Shelembi akipokea cheti katika mahafali hayo
 Emmanuel Kwitema akipokea cheti chake katika mahafali hayo ya tano
 Magomba akipokea cheti chake pia katika mahafali hayo
 PJ akipongezana na Kwitema kabla ya kutunukiwa shahada zao
PJ akiwa na wadau aliomaliza nao kupiga kitabu na kupata shahada, wakati wa mahafali hayo. Kulia ni Binti yake aitwaye Sezaria PJ.  
 Kwitema na wadau wenzake wakati wakisubiri kupata shahada zao kwenye mahafali hayo
 Unamjua Bahati Mollel mwandishi mahiri wa habari za michezo? ndiyo huyu kulia akimvisha vizuri joho mwenzake, Doris Saivoiye ambaye amewahi kuwa mwandishi wa habari na pia mhudumu katika ndege. wote wamepata Shahada ya Sanaa ya Mawasiliano ya Umma katika chuoo hicho
 Yohana Mganga akipongezwa na mama yake mdogo Bi Neema Sagamba, baada ya kupata shahada ya sheria katika mahafali hayo.
 Grace Kwitema akimpongeza mume wake, Emmanuel Kwitema kwa kutunukiwa shahada katika mahafali hayo
 Baada ya kumvisha shada la maua akampa mazagazaga kibao ya zawadi kama hivi 
Meena wa gazeti la Mwananchi (katikati) akifurahia jambo wakati wakiwa na wadau wenzake ambao wametunukiwa shahada ya sheria katika mahafali hayo.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages