Breaking News

Your Ad Spot

Nov 2, 2011

STARS KUINGIA KAMBINI KESHO KUIKABILI N'DJAMENA

Timu ya Taifa (Taifa Stars) inaingia kambini kesho (Novemba 3) kujiandaa kwa mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Chad itakayochezwa Novemba 11 jijini N'Djamena.
Wachezaji wote wanatakiwa kuripoti kambini kesho, isipokuwa wale wanaocheza mpira wa kulipwa nje ya nchi ambao wataanza kuingia nchini Novemba 4 mwaka huu.
Kambi ya Taifa Stars itakuwa hoteli ya New Africa na mazoezi yatafanyika Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam kulingana na programu za Kocha Mkuu wa timu hiyo Jan Poulsen. Timu inatarajiwa kuondoka nchini Novemba 8 usiku kwenda N'Djamena. 

Waamuzi wa mechi ambao wote wanatoka Nigeria ni Bunmi Ogunkolade, Tunde Abidoye, Baba Abel na Abubakar Ago. Mtathimini wa waamuzi atakuwa Idrissa Sarr kutoka Mauritania wakati Kamishna wa mchezo huo ni Hamid Haddadj (Algeria).
Boniface Wambura
Media Officer
Tanzania Football Federation (TFF)
Member, CECAFA Media Committee
+255 71 3210242
+255 76 7310242

1 comment:

  1. Get in our website and read more about


    [url=http://www.nauka-jezyka-angielskiego.com.pl/metody-nauczania-jezyka-angielskiego/]Nauka jezyka angielskiego[/url]

    ReplyDelete

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages