Breaking News

Your Ad Spot

Dec 1, 2011

BAADA YA CHADEMA, CUF NAO SASA WAOMBA MAZUNGUMZO NA RAIS KIKWETE

Baada ya CHADEMA kuomba na kufanikiwa kufanya mazungumzo na Rais Jakaya Kikwete kuhusu mchakato wa Katiba mpya unaoendelea, Chama Cha Civic United Front-CUF nao wameomba kufanya kama wenzao wa upinzani.
         Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Rais, Ikulu, mjini Dar es Salaam, leo, imesema kuwa Ofisi hiyo imepokea barua kutoka CUF wakiomba kukutana na kufanya mazungumzo na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete.
Mheshimiwa Rais amekubali ombi hilo la CUF na ameelekeza maandalizi ya mkutano huo yafanyike mara moja.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages