Breaking News

Your Ad Spot

Dec 16, 2011

NAPE ATWAA SHAHADA YA PILI YA UONGOZI, AFURAHIA KUTEKELEZA MOJA YA AHADI ZA MWANACHAMA WA CCM

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kmutunukiwa shahada yake ya pili ya uongozi, leo katika mahafali ya kumi ya Chuo Kikuu cha Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam, katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye (pichani) alisema, hatua yake ya kuhitimu shahada hiyo, imempa faraja kubwa kwa kuwa ametekeleza moja ya ahadi muhimu za mwanachama wa CCM, ambayo aliisoma na kuitamka wakati akikabidhiwa kadi ya CCM 

"Nilipokabidhiwa kadi ya uanachama wa CCM nilisoma kutoka katika kadi hiyo kwamba 'Nitajielimisha kwa kadiri na uwezo wangu na kutumia elimu yangu kwa faida ya wote, sasa hatua hii ya leo ni katika jitihada zangu za kuhakikisha natimiza imani hiyo", alisema Nape. 

Alisema kuwa elimu aliyoipata atahakikisha anaitumia vilivyo kwa faida ya Watanzania wote hasa katika nafasi aliyomo sasa katika siasa.
 Nape akijadili jambo na wahitimu wenzake wa Shahada ya Pili ya Uongozi wakati wa mahafali hayo. Kutoka kulia ni Meja Joseph Masanja, Magnus Mahenge na Zakia Omar
 Nape akipongezwa na Mama yake wakati wa mahafali hayo
 Watangazaji wa Chanel Ten nao wakaona lazima wampongeze Mheshimiwa Nape. Pichani, wakimpa zawadi maalum ya hongera nje ya ukumbi. Anayemkabidhi ni  Fred Mwanjala na wengine ni Salama Hamad na Zainab Abdallah
 Nape akipongezwa  na Baba yake mdogo
 Nape akiwa na wahitimu wenzake
 Nape akiwa na wahitimu wenzake muda mfupi kabla yakutunukiwa shahada zao
 Huyu jamaa ambaye ni Mkazi wa hesabu Ofisi ya Ukaguzi ya Taifa, Wilfred Gallaba, ghafla akamuona Nape, kumbe walikuwa wote kwenye mahafali hayo, naye pia amepiga nondozzz

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages