.

GARI LENYE MWANI YAZAMA BAHARINI PEMBA

Sep 30, 2011

Gari aina ya Cater lililokuwa na marobota ya mwani likiwa katika bahari baada ya kuzama hivi karibuni kisiwani Pemba. (picha na Nafisa Madai- maelezo zanzibar)
Wananchi  wakisaidia kulivuta gari hilo baada ya kuitoa baharini ilimokuwa imezama ikiwa na marobota

MKAPA ATINGA IGUNGA JIONI HII, KUFUNGA KAMPENI ZA CCM KESHO

                                                                                                                 
Mwenyekiti Mstaafu wa CCM, Rais Mstaafu Benjamin Mkapa akisalimiana
na wananchi baada ya kuwasili kwenye hoteli aliyofikia mjini Igunga
 leo jioni

 Mwenyekiti Mstaafu wa CCM, Rais Mstaafu Benjamin Mkapa amewasili jioni hii mjini Igunga.

Kufuatia kuwasili kwake, kesho atafunga kampeni za CCM katika mkutano unaotarajiwa kuwa mkubwa, kwenye Uwanja wa Sokoni, Kata ya Nkiga.

Mkapa aliwasili kwa msafara wa magari na kulakiwa naviongozi mbalimbali wa CCM mkoa wa Tabora, wakiongozwa na Katibu Mkuu wa CCM Wilson Mukama.
Baada ya kupokewa na viongozi hap msafara wa Mkapa ukipambwa na waendesha pikipiki, baiskeli, bajaji ulikwenda hadi katika hoteli maarufu ya mjini Igunga, The Peak Hotel ambako alipata mapumziko na baadaye kuwa na mazungumzo na viongozi wa Chama wa mkoa na wilaya ya Igunga.

Mkapa kufunga kampeni hizo, kutamfanya kuweka historia ya aina yake katika medani ya Siasa kwa kuwa yeye ndiye alifungua mkutano wa kampeni za CCM mjini hapa kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine.

Mbali na Mkapa kufunga kampeni katika mkutano huo, CCM pia itakuwa na mikutano mingine ya kampeni za mwisho ambayo kwa mujibu wa ratiba itafanyika Mwanzugi, Choma, Ziba, Igurubi, Uswaya na Nsimbo.

Uchaguzi mdogo jimboni hapa utafanyika Jumapili hii, baada ya kampeni za vyama vinane vinavyoshiriki uchaguzi huo ambao unafanyika kufuatia kujiuzulu aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Rostam Aziz.

HII STAILI YA TUME YA UCHAGUZI IGUNGA UNAIAFIKI?

Mama akitafuta jina lake katika orodha ya wapiga kura katika  'daftari' lililoning'inizwa kwa kufungwa na kamba kwenye nondo ya dirisha la chumba cha darasa kwenye shule ya msingi Igunga leo. Utaratibu huu wa kuning'iniza karatasi hizi, licha ya kusababisha usumbufu kwa wanaohitaji kuona majina yao kwa kulazimika kusoma mmoja mmoja, pia ni rahisi kunyofolewa na wenye nia mbaya.

UCHAGUZI IGUNGA: VIJANA WAMCHANGAMKIA DK.KAFUMU, KINA MAMA NDIO USISEME

"KULA TANO" mgombea Ubunge Jimbo la Igunga kwa tiketi ya CCM, Dk. Dalaly Kafumu (kulia) akisema hivyo wakati akisalimiana na vijana wa Kata ya Usongo, akiwa katika mkutano wakampeni za CCM za uchaguzi mdogo jimboni humo. Katikati ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Mbunge wa Mtera Livingstone Lusinde ambaye alikuwa mkuu wa msafara wa kampeni hizo.
  Dk. Kafumu akiwasalimia wananfunzi wa shule ya msingi Usongo waliojumuika kwenye mkutano wake wa kampeni uliofanyika leo katika kijiji hicho. 
Kina mama wakimlaki Dk. Kafumu aliposhuka kwenye helkopta kwenda kuwahutubia wananchi wa Mpogolo

Dk. Kafumu akivutwa huku na huko na mashabiki wake wakati akitaka kuondoka baada aya kampeni kata ya Ziba. Karibu yake ni mkuu wa msafara wake, mbunge wa Mtera Livingstone Lusinde
Lusinde akimnadi Dk. Kafumu huku wananchi wakishangilia baada ya kufika kwa helkopta jioni, katika kijiji cha Lugubu Kata ya Itumba ambako ni kijijini kwa mgombea huyo
Watu wakimsikiliza kwa makini Dk. Dalaly wakati akihutubia mkutano wa Nsimbo. Unaweza kumuona mbwa huyu naye akiwa ametulia kwa amani kutokana na mkutwnao huo kuwa wa utulivu
Dk. Magufuli akimnadi kwa raha zote Dk. Kafumu katika mkutano uliofanyika Kata ya Ziba. Watatu kulia ni Mratibu wa kampeni za CCM, Mwigulu Nchemba
Dk Dalaly na Lusinde wakichana anga kwa helkopta kwenda kwenye mikutano ya kampeni leo
Mapolisi nao hawakuwa wakicheza mbali kuhakikisha usalama unakuwa timilifu kwenye mikutano yote ya kampeni
Igunga yenyewe ndiyo hii. katikati ni barabara ya Singida-Nzega kupitia Igunga

NAPE KATIKA KAMPENI ZA UDIWANI RORYA NA TARIME

Sep 29, 2011

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, akizungumza na mabalozi wa nyumba kumi wa CCM wa tawi la Kiongera kata ya Suzuni wilaya ya Tarime mkoani Mara. 
NAPE wa pili kulia, akipokea kadi na bendera kutoka kwa wanachama wa CHDEMA waliamua kujiunga na CCM wakati wa mkutano wa kampeni katika Kijiji cha Nyabirongo Kijiweni kata ya Suzuni, Tarime mkoani Mara. Kutoka kushoto ni Juma Marwa, Amos Marwa na John Wanguru. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa wilaya ya Tarime, Bogomba Chichake. 
NAPE akihutubia mkutano wa kampeni Kijiji cha Nyabirongo Kijiweni. 
NAPE akiwasha mwenge alipowasili Kijiji cha mpakani kati ya Tarime na Rorya cha Bakwe, kuanza ziara wilayani Rorya 
 NAPE akikagua ujenzi wa ofisi ya CCM kata ya Bakwe, wilaya ya Rorya mkoani Mara. 
WANANCHI wa Kijiji cha Rwang’enyi, wakimshangilia Nape alipohutubia mkutano wa kampeni kumnadi mgombea udiwani wa CCM wa kata ya Naymtinga, kijijini hapo 
NAPE akipiga ngoma ya kikundi cha sanaa kilichtumbuiza wakati wa mkutano wa kampeni katika Kijiji cha Rwang’enyi. 
 NAPE akihutubia mkutano wa kampeni kmnadi mgombea udiwani wa kata ya Nyahongo wilaya ya Rorya kwa tiketi ya CCM, Mussa Aago.
NAPE akimnadi mgombea udiwni wa kata ya Nyahongo kwa tiketi ya CCM, Mussa Aago, wakati wa mkutano wa kampeni katika Kijiji cha Omoche, wilaya ya Rorya mkoani Mara.

MWILI WA POLISI ALIYEUAWA KIKATILI MBEYA WAAGWA

Sep 28, 2011

KAIMU Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Evans Balama, akizungumza leo wakati wa kuuga mwili wa askari polisi G.2795 PC Meshack Urrasa, aliyeuawa kwa kupigwa nondo na watu wasiofahamika eneo la Mabatini mjini Mbeya.

NAKAGAWA AMUAGA JK

Rais Jakaya Kikwete akiagana na Balozi wa Japan hapa nchini anayemaliza muda wake, Mheshimiwa Hiroshi Nakagawa, ambaye alienda ikulu kuagana na Rais Kikwete leo. Picha na John Lukuwi

MAMBO YA TASWA USIPIME!

KAMATI ya Utendaji ya Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) imeteua washiriki 40 kwa ajili ya mafunzo ya waandishi wa habari za michezo yatakayofanyika mkoani Morogoro kuanzia Septemba 30, 2011 hadi Oktoba 2, 2011.
        Washiriki wataondoka Dar es Salaam, Ijumaa saa 8 mchana kwa usafiri wa pamoja na watarejea Jumapili Oktoba 2, 2011 baada ya mafunzo kufungwa saa 10 alasiri.Uteuzi umezingatia zaidi wale ambao hawakuwahi kushiriki mafunzo yoyote yaliyoandaliwa na TASWA na pia umezingatia mahitaji ya chombo husika cha habari. 
        Pia umezingatia mafunzo mengine yatakayofanyika Novemba mwaka huu mkoani Arusha, ambayo yatakuwa na idadi kubwa ya washiriki.
          TASWA inaishukuru kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania kwa kuwa mdhamini mkuu wa mafunzo haya, pia kampuni ya mabasi ya Al Saedy kwa kuwa mdhamini mwenza, tunaamini mchango wao ni mkubwa zaidi.
          Mafunzo yataegemea zaidi masuala ya maadili ya uandishi wa habari, mambo ya uandishi wa makala za michezo na masuala yahusiyo sheria za michezo mbalimbali nchini. Walioteuliwa na vyombo vyao katika mabano ni Zaituni Kibwana (Bingwa), Olipa Assa (Dimba), Jennifer Ulembo(Mtanzania), Sweetbert Lukonge (Mwananchi), Doris Malyaga (Mwanaspoti) na Suleiman Jongo (The Citizen).         
        Wengine ni Renatha Msungu (Nipashe), Steve Wills (The Guardian), Maulid Kitenge (Redio One), Jimmy Tara (ITV), Master Tindwa (Capital Redio), Hassan Mvula (Star TV/Redio Free),  Alex Luambano(Clouds Media), Mbozi Katala (TBC1), na Shadrack Peter (Chanel Ten).Pia wapo Sigori Paul (Redio Uhuru), Crecensia Tryphone (Tanzania Daima), Japhet Kazenga (Daily News), Crecence Kunambi (HabariLeo), Adolph Bruno (Majira), Shaaban Mbegu (Spotistarehe),  Shaaban Kondo (Times FM),  Hamis Shimye (Uhuru), Erasto Stanslaus (Mseto), Ezekiel Kitula (Championi), Selemani Mkangara (Changamoto), Salome Milinga(JamboLeo) na Anwar Mkama (Mlimani TV).
          Wanaotoka Pwani ni Omary Mngindo na Masau Bwire, wakati wa Morogoro ni Nickson Mkilanya, Idda Mushi,Ratifa Ganzel Uhuru,  John Nditi, Abeid Dogoli,Titus Munga, Ramadhan Libenanga, Samuel Msuya, Jimmy Mengele na Lilian Lucas.
                           Nawasilisha,  Amir MhandoKatibu Mkuu TASWA28/09/2011

HELKOPTA YA KAMPENI ZA CCM YATUA IGUNGA, MAGUFULI, JANUARI WATIA TIMU

Helkopta ikitua katika Uwanja wa Sabasaba mjini Igunga leo 
Januari Makamba akilakiwa na Kiongozi wa kampeni za CCM Igunga, Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha Mwigulu Nchemba. Kushoto ni Katibu Msaidi Mkuu Itikadi na Uenezi Sixtus Makamba 
Kisha Januari akakumbatiana na Mwigulu 
Januari akisalimia mamia ya wananchi kwenye Uwanjahuo wa Saba saba 
Magufuli akiwavulia kofia wananchi kuwasalimia kwenye uwanja huo  
Dk. Magufuli akijadiliana jambo na Dk. Dalaly m
agufulimD
Dk. Magufuli akimnadi Dk. Dalaly kwenye Uwanja huo wa Saba saba 
Dk. Magufuli akiwa kwenye jukwaa na viongozi wa kampeni za CCM 
Mamia ya watu wakishangilia kwneye viwanja vya Sabasaba mjini Igunga 
Ikawa ni raha tupuuuuuuuu 
Dk Magufuli akimuombea tena kura mgombea wa CCM. Kulia ni Katibu wa NEC Oganaizesheni Asha Abdallah Juma

CUF WALIA KUFUATWA FUATWA NA CHADEMA KWENYE MIKUTANO YAO YA KAMPENI IGUNGA

Sep 27, 2011

NA MWANDISHI WETU, IGUNGA
Ntatiro na Magdalena Sakaya wakizungumza leo Igunga

Chama Cha Wanachi (CUF) kimewakemea CHADEMA na kuwataka kuacha siasa za vurugu na kuwafuata fuata kwenye mikutano yao ya kampeni.
Hayo yalisemwa LEO na Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Julius Ntatilo katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika mjini Igunga.
Alisema katika kudhihirisha kuwa CHADEMA ni makamanda wa siasa za vurugu na fujo, wamekuwa wa wakiwafuata fuata CUF kwenye mikutano yao mbalimbali ya kampeni jambo ambalo amesema linakera mno na ni ishaara ya kutafuta maafa.
"Ipo mifano ya wazi kwa hawa CHADEMA kutufutana fuata, kila tunakokuwa na mikutano wanakwenda na gari lao na kuliegesha karibu kabisa na mahali tulipo, haya yalitokea pale Itumba, Nanga na mahali pengi zaidi ya mara nne", alisema Ntatilo.
"Juzi nikiwa na mkutano pale Nanga , watu wawili wakiwa na magwanda ya CHADEMA walikuja na kuingia kabisa kwenye mkutano wetu, eti wakajidai kunisalimia. Hebu niambieni watu wakivaa sare za chama kingine kama CUF au CCM wakiingia mkutano wa CHADEMA wanaweza kusalimika?" aliuliza Ntatilo.
Alisema, baada ya kujidai kumsalimia kwenye mkutano huo, Ntatilo aliwafukuza kistaarabu na kuwataka wasirudie tena utaratibu wao huo mbaya na wa kichokozi.
"Naomba sana katika siku hizi chache zilizobaki CHADEMA wajaribu kuwa wastaarabu ingawa naamini hawawezi, hizo fedha zao wanazogawa wagawe huko huko, wananchi wa Igunga wanachotaka ni uchaguzi wa amani na utulivu siyo magomvi", alisema Mtatilo.
Alisema, vyama vitakavyoendeleza vurugu wakati wa uchaguzi vitakuwa vimechuma dhambi kubwa, kwa sababu baada ya uchaguzi inatakiwa abaki mbunge siyo kuwaachia vifo wananchi wa Igunga.
Kuhusu CHADEMA kuwaita CUF CCM B, Ntatilo alisema, tuhuma hizo ni za kitoto na dalili kwamba CHADEMA hawajui siasa za kistaarab.
" Sisi tulikuwa chama cha vurugu hakuna asiyejua, lakini imefika mahali tukaona kwamba hatuwezi kuendelea kuwa chama cha upinzani tu, lakini lazima tushike dola, sasa tumepata fursa tumepata pale Zanzibar, badala ya kutupongeza hawa CHADEMA wanatukejeli, hawa wanaakili kweli?" alisena Ntatilo.
"Yaani walitaka hata baada ya kufikia maelewano kwamba kuwepo na serikali ya Kitaifa, basi tukatae kila kitu na kuendelea kuwa ngangari tuuuu' ahhh' haiwezekani hicho kitakuwa ni chama kilichokuwa na lengo baya kwa nchi si CUF", alisema.
Katika hatua nyingine Ntatilo ameshusha tuhuma kwa CCM kwamba imeingiza 'janjawidi' kwa ajili ya kufanya fujo wakati wa uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Jumapili wiki hii.
Hata hivyo CCM imekanusha vikali na kusema kwamba, haiwezi kufanya hivyo, na kwaamba vijana waliopo ni kwa ajili ya kulinda usalama wa viongozi na wanachama wa CCM na vijana hao siyo siri wanajulikana.
Mratibu wa kampeni za CCM, Mwigulu Nchemba alisema, ili kujiweka tayari na kuhakikisha inao vijana wa kutosha katika kusimamia baadhi ya shughuli kama za uwakala wakati wa uchaguzi imewap[a mafunzo ya kikakamavu na ya kujenga akili na siyo ya kijeshi kama inavyopotoshwa.
Wakati huohuo, Katibu wa NEC, Oganaizesheni CCM, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Asha Abdallah Juma, amewataka viongozi wote wa CCM kuhakikisha hakuna mwana-CCM anajitokeza kupiga kura Jumapili.
Akizungumza kwenye mkutano wa kampeni za CCM kwenye kijiji cha Ipumbulya,Kata ya Bukoko jimboni hapa, Asha alisema, kimsingi CCM inao wanachama wengi na hata mikutano ya kampeni imedhihirisha hilo kwa hiyo hakuna sababu itakayoifanya CCM ishindwe wanachana, wapenzi na wakereketwa wote watajitokeza kupiga kura.
Asha alisema, serikali ya Chama Cha Mapinduzi itahakikisha unakuwepo usalama wa kutosha katika maeneo yote tangu majumbani, njiani na kwenye vituo vya kupiga kura hivyo mtu yeyote asihofu kutoka akidhani yupo atakayemdhuru.
Naye Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Steven Wasira amesema hakuna chama chochote cha Siasa ambacho kimeweza kuonyesha hadi sasa kuwa kinaweza kuwa mbadala kwa CCM.
Akimnadi mgombea ubunge wa Igunga kwa tiketi ya CCM, Dk. Dalaly Kafumu, Wasira ambaye ni Mbunge wa Bunda alisema, ni kosa kwa sasa mtu yeyote kudhani kuwa kipo chama chenye uwezo kama CCM katika kuongoza wananchi kwa kuwa havijawa na sera makini.
"Vyama hivi vikija hapa mwanzo wa mkutano hadi mwisho ni matusi weee mpaka basi, na wakijaribu kutoa sera wanakopi zile zile za CCM ambazo wao hawawezi kuzitekeleza kwa kuwa haziwahusu" alisema Wasira.

JK AREJEA NCHINI KUTOKA US

Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete  akisalimiana na Waziri Mkuu Mizengo Pinda muda mfupi baada ya kuwasili kutoka New York Marekani ambapo pamoja na mambo mengine  alihutubia baraza la Umoja wa Mataifa.Kushoto no Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadik(picha na Freddy Maro).

BAADHI YA MATUKIO MDAHALO WA WAGOMBEA UBUNGE IGUNGA

Sep 26, 2011

Wagombea Ubunge jimbo la Igunga, Dk Dalaly Kafumu -CCM (kijanai), Joseph Kashindye -CHADEMA (kaki) na  Leopold Mahona-CUF (Bluu) wakipongezana baada ya mdahalo wao uliofanyika usiku wa kuamkia leo mjini Igunga.
 Naibu Katibu Mkuu wa CUF Julius Ntatiro, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Mwigulu Nchemba na Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Zitto Kabwe wakiwa kwenye mdahalo huo.
 Polisi akiwatuliza watu wenye munkari waliotaka kuvuruga mdahalo huo kabla ya kuanza
Zitto Kabwe akimvuta mkono Mbunge wa Tabora mjini, Alhaj Aden Rage kumpeleka safu ya mbele kutoka nyuma alikokuwa amekaa. Aliamua kumhamisha baada ya kufanyiwa zogo mara kwa mara ya wafuasi wa CHADEMA
Wagombea wakisubiri kujibu maswali wakati wa mdahalo huo
Mmoja wa wananchi waliohudhuria akiluza maswali wagombea wakati wa mdahalo huo

BEI ZA MFUTA KUANZIA KESHO HIZI HAPA

Sep 25, 2011

Product
Retail Price (TZS/L)
Wholesale Prices (TZS/L)
Using Old Formula
Using New Formula
Using Old Formula
Using New Formula
Petrol
2,291.55
2,101.67
2,223.30
2,034.17
Diesel
2,184.26
1,999.05
2,111.70
1,931.55
Kerosene
2,152.54
1,966.66
2,079.98
1,899.16

 Imetolewa na Mamlaka ya Usimamizi wa Nisahti na Maji (EUWURA) Sept 26,2011

SAKATA LA DC IGUNGA: SASA BAKWATA WATAKA CHADEMA WANYIMWE KURA

Sep 23, 2011

NAPE AZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI JIJINI MWANZA LEO

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye, akizungumza na waandishi wa habari, Ofisi ya CCM mkoa wa Mwanza leo.

RAIS KIKWETE APATA TUZO MBILI

Sep 22, 2011

Rais Jakaya Mrisho Kikwete jana (21 Septemba, 2011) amepokea Tuzo Mbili Maalum kwa mchango wake mkubwa katika Afya ya Mama Mjamzito na Watoto kwa ujumla kutoka taasisi mbili tofauti mjini New York.
Tuzo ya kwanza imetolewa na Taasisi ya Kijamii ya Umoja wa Mataifa (UN Foundation) na kukabidhiwa kwa Rais na Makamu wa Rais wake anayeshughulikia sera ya Umma Bw. Peter Yeo.
Rais amepokea Tuzo ya pili katika makao makuu ya Soko la Hisa la Marekani (National Association of Securities Dealers Automated Quotations) kwa kifupi NASDAQ ambalo ni soko la pili kwa ukubwa duniani baada ya lile la New York.  Rais amekabidhiwa tuzo hiyo na Makamu wa Rais wa NASDAQ Bw. David Wicks.
 Mara baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo Rais amepewa heshima maalum ya kugonga kengele kuashiria mwisho wa biashara kwa siku hiyo.
Akipokea tuzo hizo mbili maalum, Rais ameelezea changamoto zinazoikabili sekta ya Afya nchini Tanzania na Afrika kwa ujumla na kuzishukuru nchi na taasisi mbalimbali ambazo zinaunga mkono juhudi za kupunguza matatizo ya afya ya mama mjamzito.
Si sahihi kwa mama mjamzito kufariki wakati anampa uhai binadamu mwingine, uzazi unatakiwa kuwa shughuli ya furaha na sio huzuni na ndiyo maana tumetoa kipaumbele kwenye afya ya mama mjamzito kwenye ajenda yetu ya Afya” Rais amesema.
Rais amewaeleza wageni waalikwa ambao katika hadhara zote mbili wametoka katika nchi na taasisi mbalimbali kuwa kati ya vitu ambavyo serikali ya Awamu ya Nne imeamua kutoa kipaumbele katika kuongeza huduma za afya ya uzazi kwa kujenga zahanati na kuzipandisha daraja zilizokuwepo.
Serikali pia inaajiri wakunga na wataalamu zaidi wa Afya na kuongeza mafunzo katika sekta hiyo.
Juhudi zingine ni pamoja na kutoa huduma za Mpango wa Uzazi bure na kutoa vifaa vya kujifungulia kwa akina mama wanaohudhuria kliniki.
Vifaa hivi ni maalum kwa ajili ya kuwasaidia akina mama wakati wa kujifungua, na tuna amini kuwa kwa kufanya hivi wanawake wengi zaidi watahudhuria kliniki na kuwapa motisha wa kujifungulia katika taasisi zetu za afya”. Rais ameeleza.
Kutokana na juhudi hizo takwimu zinaonyesha kupungua kwa vifo vya akina mama wajawazito na  wakati wa kujifungua  kutoka 8,000 kwa mwaka 2005 hadi 6,000 mwaka jana.
Upungufu wa vifo 2,000 ni hatua nzuri katika muda mfupi lakini bado hairidhishi sana, tunaweza kupunguza zaidi na hilo ndiyo lengo letu kwani hatutaki kuona mwanamke yeyote anakufa kutokana na ujauzito au wakati wa kujifungua”. Rais amesema.
Mbali na shughuli hizo, Rais amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Slovenia Dr. Danilo Turk, Makamu Waziri Mkuu wa Luxembourg Bw. Jean Asselborn na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki Moon na Waziri wa Maendeleo wa Uingereza Bw. Andrew Mitchell.
Leo tarehe 22 Septemba, 2011, Rais anatarajiwa kuhutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

Imetolewa na Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
New York.
Marekani.
22 Septemba, 2011

MAANDALIZI TAMASHA LA KWANZA LA BIA TANZANIA

      Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager Bw. George Kavishe (katikati) akizungumza na     Waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam jana kuhusu Tamsha la Kwanza la Bia Tanzania lililoandaliwa na Kilimanjaro Premium Lager and Kampuni ya Bongo 5 mwezi ujao. Kushoto ni Mratibu wa Matukio wa Bongo 5, Olive Nimaga na kulia ni Afisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania, Dorris Malulu.

MUKAMA ATEMA CHECHE IGUNGA

Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama akizungumza na waandishi wa habari leo,katika Ofisi ya CCM wilaya ya Igunga mkoani Tabora, kueleza tathmini na mwenendo wa kampeni za CCM za uchaguzi mdogo jimbo la Igunga. Kulia ni Katibu wa Halmsahauri Kuu ya Taifa ya CCM, Oganaizesheni Asha Abdallah Juma.
      Akizungumzia tathmini alisema kampeni zinaenda vizuri na CCM inaonyesha kuwa inaungwa mkono na wananchi wengi wa Igunga na hivyo inatarajia ushindi wa uhakika uchaguzi utakapofanyika Oktoba 2, mwaka huu baada ya kampeni.
     Pia ametumia nafasi hiyo kuvitaka vyombo vya habari kuandika habari zao kulingana na taaluma inavyowataka badala ya kuandika uongo kwa maslahi ya vyama wanavyopendelea au wanavypenda wao iwe.
    Mukama aamelaani na kutangaza hadharani kwamba CHADEMA wameleta makomandoo jimbo ni na kuwasambaza katika kata kadhaa kwa lengo la kutosha wananchi na kufanya fujo katika kampeni zinazoendelea na wakati wa uchaguzi.
      Akitaka kata walimo makomandoo hao, Mukama amesema pia wengi wao wamepata mafunzo nchi za nje. Hata hivyo alikataa kuwataja majina ili kuiwezesha serikali kufanyia kazi kikamilifu taarifa ambavyo CCM imeripoti kuhusu hali hiyo.

CCM YAZIDI KUPENDWA IGUNGA, NYOMI YA WATU MKUTANO WA MWANZUGI KATA YA IGUNGA VIJIJINI YATIKISA

Nyomi ya watu kwenye mkutano wa kampeni za CCM eneo la Mwanzugi, Kata ya Igunga Vijijini, jana. 
   Mgombnea wa CCM, Dk. Dalaly Kafumu akihutubia  nyomi ya wananchi kwenye mkutano wa kampeni za CCM, eneo la  Mwanzugi Kata ya Igunga Vijijini, mkoani Tabora, jana.
    Mratibu wa kampeni za CCM Igunga, Mwigulu Nchemba akihutubia maelfu ya watu, kijiji cha Mwanzugi Kata ya Igunga Vijijini jana
 Khadija Kopa, Dk.Kafumu, Nchemba na Lusinde wakishambulia jukwaa.. 
    Khadija Kopa wa TOT akihamasisha kwenye mkutano wa CCM eneo la Mwanzugi . 
Mgombea wa CCM Dk. Kafumu akiwaaga wananchi baada ya mkutano huo
ยช