Breaking News

Your Ad Spot

Jan 29, 2012

AJALI YAUA WATANO NYOLOLO, IRINGA

Watu watano wamekufa na wengine 16 kujeruhiwa baada ya basi la kampuni ya New Force lenye namba T666BCR kupinduka, eneo la Nyololo wilkayani Mufindi mkoani Iringa, jana.

Taarifa ambazo blogu hii imezipata muda si mrefu zimesema basi hilo lilikuwa inasafiri kwenda Kyela mkoani Mbeya likitokea jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa habari hizo watu wanne walikufa papo hapo na mmoja akiwa katika chumba cha upasuaji katika hospitali ya Mafinga.

Taarifa za Polisi zimnesema dereva wa basi hilo Yahya Abdallah anatafutwa na jeshi hilo baada ya kutoroka baada ya ajali hiyo ambapo inadaiwa ilisababishwa na dereva huyo.

Inaelezwa kwamba katika ajali hiyo, magari mengine mawili moja lenye namba za usajili STK 2340 na lingine ambalo namba zake hazikujulikana mara moja yaligongana na lori yakijaribu kulikwepa basi hilo lililopinduka.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages