NA MWANDISHI WETU
Maadhimisho ya miaka 35 ya CCM yanazinduliwa nchini kote kesho, Januari 30, na shamra shamra zake kuendelea kwa matukio mbalimbali hadi Jumapili ijayo, Februari 5, yatakapofikia kilele.
Akizungumza katika kipindi cha tuongee asubuhi kilichorushwa moja kwa moja leo asubuhi na Kituo cha Televisheni cha Star Tv, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alisema kwa jumla maandalizi ya sherehe hizo yamekamilika.
Nape alisema, baada ya uzinduzi huo, siku nne zitakazofuatia kuanzia Januari 31, zitatumika kufanya shughuli mbalimbali za Jumuia za Chama (Umoja wa Vijana wa CCM-UVCCM, Jumuia ya Wazazi na Umoja wa Wanawake Tanzania-UWT).
Alisema, Februari 4, Siku moja kabla ya kilele cha maadhimisho hayo, matawi yote ya CCM nchini yatafanya shughuli muhimu ya kutathmini uhai na uhalali wa wanachama katika matawi yao.
"Hii ni shughuli muhimu sana, kwa Chama kinataka kuhakikisha baada ya tathmini hiyo kinaondokana na wanachama wale wa dharura kama kiliowapata wakati wa kura za maoni kupata wagombea wakati wa uchaguzi mkuu uliopita, ambao kimsingi wamekuwa moja ya matatizo ndani ya Chama", alisema Nape.
Alisema, siku ya kilele, Jumapili Februari 5, jijini Mwanza ambako maadhimisho yanafanyika kitaifa, Mweneyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete ataongoza matembezi ya mshikamano asubuhi na jioni itafuatia sherehe kubwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba ambako Rais Kikwete na Wenyeviti wastaafu wa CCM watahudhuria.
"Nimeshapata taarifa kutoka kwa wenzangu wa Mwanza kwamba heshima hii waliyopewa wameipokea kwa shangwe kubwa na kwamba hadi sasa wameshafanya maandalizi makubwa kuhakikisha sherehe za kilele cha maadhimisho hayo zinakuwa za kihistoria kwa kufana", alisema Nape aliyekuwa akizungumza kutoka studio namba mbili za Star Tv jijini Dar es Salaam.
Nape aliwataka wananchi wa Mwanza kujitokeza kwa wingi kwenye Uwanja wa CCM Kirumba kwenye sherehe hizo, kwa kuwa mbali na kwamba watakuwa wanapokea heshima ambayo mkoa wao umepwa, pia watajionea mambo mengi zikiwemo burudani zitakazotolewa na vikundi mbalimbali mahiri nchini.
MASWALI
Akijibu kiongoni mwa maswali yaliyoulizwa na waongozaji wa kipindi hicho, James Rangr (Dar es Salaam) na Bernard James (Mwanza), Nape alisema si kwelie kwamba CCM katika uhai wake wote wa miaka 35 haishughuliki kuleta hali bora za maisha ya watu.
Nape alisema, kwa mfano CCM imekuwa ikisimamia na kutafuta ufumbuzi kukabiliana na mfumuko wa bei za bidhaa ili kupunguza makali ya maisha ya Watanzania licha ywa kwamba baadhi ya watu wanabeza.
Alisema, wakati Tanzania inakabiliwa na mfumuko wa kupanda kwa gharama za maisha, katika nchi za Uganda na Kenya mfumuko huo ni mkubwa kuliko Tanzania.
"Hili la mfumuko watu wanalitumia kisiasa, lakini kwa kweli haliihusu Tanzania peke yake, ni la dunia nzima. Ukitazama hali ya mfumuko wa gharama za maisha Kenya na Uganda ipo juu kuliko Tanzania, na hii si kwamba Tanzania ina unafuu kuliko nchi hizo kwa sababu ya bahati la hasha kuna juhudi zinafanywa, ukiona vinaelea vimeundwa", alisema Nape.
Kuhusu suala la kura za maoni uliotumika kuwapata wagombea wa CCM katika ngazi mbalimbali ukiacha urais, wakati wa uchaguzi mkuu, Nape alisema wana-CCM wengi wameonyesha kuupenda, lakini unafanyiwa maboresho kuthibiti mapungufu yanayosababishwa na mfumo huo.
"Hili ni swala la kidemokrasia hatutaliacha, tutaliboresha kuondoa mapunfugu yaliyojitokeza moja wapo ni kuhakikisha tunaziba mianya ya kuzalisha wanachama bandia kwa ajili ya kupiga kura ambao walijitokeza sana wakati wa uchaguzi mkuu uliopita", alisema Nape.
Kuhusu lililoulizwa na wasikilizaji na pia mwongozaji wa kipindi hicho, Range, kwamba ndani ya CCM kuna watuhumiwa wa rushwa ambao bado wanapeta, Nape alisisitiza kwamba hakuna mla rushwa atakayesalimia, isipokuwa ni utaratibu tu wa kuwashughulikia ambao pengine unaonekana kama ni wa pole pole mno.
"Hawa wote wanashughulikiwa, kwa sababu taratibu zinazosimamia kushughulikiwa kwa wala rushwa zipo na zimeandikwa katika katiba na imani za Chama, hazijabadilika, isipokuwa utaratibu wenyewe wa kuwashughulikia labda ndio pengine watu wanaona ni wa polepole mno na hili ikiwa ndiyo kikwazo basi litajadiliwa na kuwekwa utaratibu mwingine wa kushughulikiana haraka", alifafanua Nape na kuongeza.
"Tatizo linalojitokeza ni kwamba tunaposimama na kusema kwamba fulani ni mla rushwa au si mwadilifu awajibike, yanaaza kuzuka maneno kwamba tunatisha watu, Kwenye vyombo vya habari nimesoma kwamba Mimi Nape natisha watu.. mimi jamani sitishi watu maneno ninayosema kila siku kuhusu watu hawa yameandikwa katika katiba na kanuni za Chama, si yangu".
"Kwanza inasikitisha kwamba wakati mwingine watu waonafuja mali za umma na kula rushwa wakiwa ni viongozi waliopewa dhamana chini ya Chama tunawaita majina mepesi mepesi, kwa kweli hawa kwa kuwa ni watu wanaokiuta katiba na imani ya Chama ni wasaliti tu", alisema Nape.
Ajibu swali kuhusu azma ya kutenganishwa siasa na biashara, Nape alisema dhana hiyo, inaendelea kufanyiwa kazi ndani ya Chama, lakini pia serikali imeombwa kuopitisha itungwe sheria itakayoainisha moja kwa moja uthibiti huo.
"Siyo siri kwamba matumizi makubwa ya fedha katika uchaguzi yameingizwa na wafanyabiashara, kimsingi wafanyabiashara si vibaya kuwa wanasiasa lakini sasa Chama kimeona ni lazima sasa utaratibu wa kudhibiti uwezo wao wakitaka kukiuka. Hata enzi za Mwalimu Nyerere walikuwepo wafanyabiashara katika siasa lakini hazikutumika fedha kama tunavyoshuhudia sasa", alisema Nape.
Kuhusu wanaokimbizana kutengeneza njia ya kuwawesha kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya CCM, Nape alisema, wanapoteza muda wao kupanga harakati zao kwa sasa kwa kuwa baada ya Machi Mwaka jana Sekretarieti mpya kuundwa iliundwa tume ya siri ya kuratibu njia bora itakayowezesha CCM kupata mgombea bora.
Alisema, kutokana na hali hiyo, wanaotumia mbinu mbalimbali kwa sasa wanapoteza muda wao kwa kuwa upo uwezekano mkubwa tume hiyo ya siri ikaja na utaratibu ambao anaamini utakuwa tofauti na njia wanazodhani zitawafaa wanaotaka kuwania urais.
Wakati katika kipindi hicho, Nape alikuwa studio za Dar es Salaam, jijini Mwanza walikuwepo makada wa CCM, Frank Uhahula na Bituro Kazeri ambao walishiriki kwa umahiri mkubwa kujibu na kufafanua hoja mbalimbali zilizoulizwa.
Your Ad Spot
Jan 29, 2012
Home
Unlabelled
MAADHIMISHO MIAKA 35 YA CCM KUZINDULIWA KESHO: NAPE AZUNGUMZA STAR TV LEO
MAADHIMISHO MIAKA 35 YA CCM KUZINDULIWA KESHO: NAPE AZUNGUMZA STAR TV LEO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269