Breaking News

Your Ad Spot

Jan 6, 2012

NAPE AMPONGEZA MNYIKA KUPEWA UENZI WA CHADEMA

Akizungumza leo mjini Dar es Salaam, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye amesema anampongeza sana John Myika kuteuliwa na Chadema kuwa Mkuu wa Habari na Uenezi wa chama hicho.

"Nasema hatua ya Chadema kumchagua Mnyika kushika nafasi hiyo ni nzuri kwa kuwa imeonyesha nijinsi gani vijana wanaendelea kuaminiwa na kupewa nafasi muhimu za uongozi", alisema Nape na kumkaribisha Mnyika katika ulingo wa viongozi wa Uenezi katika vyama vya siasa.

Katika picha ni Nape na Mnyika walipokuwa katika kongamano la kisiasa lililofanyika hivi karibuni ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages