Breaking News

Your Ad Spot

Jan 6, 2012

WATANO WAPIGWA PANGA KOZI YA NGUMI

Rajabu Mhamila mmoja wa makocha waliopenya
Na Mwandishi Wetu
SHIRIKISHO la Ngumi za ridhaa nchini (BFT) limepiga panga majina matano kati ya 30 ya makocha walioteuliwa kushiriki katika kozi ya kimataifa ya mchezo huo iliyopangwa kufannyika Januari 16 mwaka huu.

BFT imewakata washiriki hao baada ya Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) kuwataka BFT kupunguza idadi ya washiriki kutokana na hasara iliyosababishwa na washiriki hao katika kozi ya awali iliyokuwa ifanyike tangu mwezi Novemba mwaka jana.

TOC ambayo huandaa kozi za michezo mbalimbali kutokana na ruzuku inayotolewa na Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa (IOC) ilikuwa iendeshe kozi hiyo tangu mwaka jana lakini haikufanyika kutokana na mkufunzi wa kozi hiyo kutoka nchini Algeria kuingia mitini.

TOC ililazimika kuwalipa nauli baadhi ya washiriki waliotoka nje ya Dar es Salaa kutoka katika fungu la pesa   za kuendeshea kozi hiyo hivyo kuwataka BFT kupunguza idadi ya washiriki hasa wale waliofanya
utovu wa nidhamu katika kozi ya awali ili kiwango cha pesa kilichobaki kutosheleza mahitaji ya kozi hiyo ya Januari 16.

Akizungumza Dar es Salaam Katibu mkuu wa BFT, Makore Mashaga alisema idadi ya makocha 25 waliowateua inaweza ikapungua tena kulingana na bajeti waliyobaki nayo TOC ambapo hata hivyo hakuyataja majina matano ya washiriki walioachwa .

Aliwataja washiriki waliopenya kuhudhuria kozi hiyo ni mpiga picha wa Magazeti ya Busines Time, Majira, Sports Starehe na Jarida la Maisha ambaye pia alikuwa bondia, Rajabu Mhamila 'Super D', Anord Ngumbi,
Moses Lema,  Anthon Mwang'onda na Edward Emanuel (Dar es Salaam).

Wengine ni Yahaya Mvuvi (Tabora), Joseph Mayanga na Zakaria Mwaseba (Morogoro), Omari Saady na Mussa Bakari (Mwanza), Ally Ndee (JKT Mbeya), Emilio Moyo na Gaudens Uyaga (Pwani) Juma Liso (Magereza Kigoma), Lyinda Kalinga (Dodoma) na Abdalah Bakari  (Tanga).

Alitaja  wengine ni  Mohamed Hashim  (Polisi Dar es Salaam), David Yombayombam, Haji Abdalah, Said Omari (JWTZ),  Mazimbo Ally, Rogated Damian na Fatuma Milanzi (JKT), Musa Maisori na Hamisi Shaaban Magereza Dar es Salaam).

Kozi hiyo itaendeshwa na mkufunzi wa kimataifa Josef Diouf kutoka Shirikisho la Dunia la mchezo huo (AIBA) ambaye atashirikiana na makamu wa Rais wa BFT, Michael Changarawe.

Kozi hiyo itafanyika  shule ya Sekondari ya Filbert Bayi Kibaha Mkoani Pwani  na itafikia tamati  Januari 24 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages