Breaking News

Your Ad Spot

Feb 28, 2012

MAWAZIRI WAKUTANA MAREKANI KUJADILI HALI YA WANAWAKE WA VIJIJINI


NA Mwandishi Maalum
New  York

Mawaziri wanaohusika na masuala ya maendeleo ya wanawake kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, wameanza mkutano wao wa wiki mbili ambapo watajadiliana na kubadilishana mawazo kuhusu    hali ya wanawake hasa wale wa vijijini.
Mkutano huo  ambao  ni wa 56 umeandaliwa na   Tume ya Umoja wa Mataifa  kuhusu   Hali ya Wanawake   na umefunguliwa rasmi siku ya jumatatu na  Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dk. Asha-Rozi Migiro hapa  Makao Makuu ya  Umoja wa Mataifa, Jijini New York, Marekani
Mada kuu ya mkutano huo   ni “ nafasi ya  wanawake wa vijijini na  mchango wao katika kupambana na umaskini na njaa. Na namna   gani wanaweza kuwezeshwa ili wapate nguvu ya kuwa kichocheo cha maendeleo endelevu”.
Ujumbe wa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika  mkutano huu unaogozwa  na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe. Sophia Simba ( Mb)  akiwamo pia Mhe. Zainabu Omar Muhamed(Mb)  Waziri wa  Jamii na Maendeleo ya  Vijana, wanawake na Watoto kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Wengine waliomo katika ujumbe huo wa Tanzania, ni  Bibi Kijakazi Mtengwa,  Katibu Mkuu  Wizara ya    Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe. Iman Daud  Aboud, Jaji Mahakama ya Rufaa,  Bi Rahma Ali Khamis, Mkurugenzi wa  Jinsia kutoka  Zanzibar,  Bw. Francis Ali Khamis  Mtungi, Msajiri wa Mahakama ya Rufaa.,Bibi Grace Job Mbwilo,1 | Page  Afisa Maendeleo ya Jamii  Mwandamizi   Wizara ya  Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto , Bibi Joyce Mlowe kutoka Wizara ya Katiba na Sheria na  Bibi Teodosia  Mbuda, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na  Watoto
Akifungua mkutano huo, Naibu Katibu Mkuu ameeleza kwamba kama wanawake wa  vijijini wangepewa fursa sawa  ya kupewa nyenzo za  uzalishaji, hapana shaka   uzalishaji wa mazao ya kilimo ungeongezeka maradufu na   kiwango cha njaa kingeshuka.
Hata hiyo anasema Migiro “ ukweli ni kwamba wanawake wa vijijini na wasichana  wanaendelea kukabiliwa na vikwazo vingi vikiwamo ya upatikanaji wa ardhí, pembeje za kilimo, mitaji ya fedha , huduma na ugani na teknolojia za kisasa”
Na kuongeza kwamba, bado wanawake wa vijijini wanaendelea kukabiliwa na  ugumu  katika upatikanaji wa  huduma za msingi zikiwano za  ulizi wa jamii, ajira na masoko ya uhakika.
 Na kwa sababu hiyo ametoa wito kwa wajumbe wa mkutano huo  kujadiliana kwa kina   kuhusu mikakati itakayowawezsha wanawake wa maeneo ya vijijini kuongeza uwezo wao wa kupambana na umaskini uliokithiri, njaa na kujiletea maendeleo endelevu katika familia zao.
Aidha Migiro anasema kwamba  ili hayo yote yaweza kufanikiwa kwanza ni lazima jamii  itambue kwamba wanawake ni mawakala muhimu wa mabadiliko. Na kwamba wakisaidiwa katika jumuia zao kutasaidia sana katika kuhakikisha kwamba ,matakwa na vipaumbele vya wanawake wa vijijini  yanapewa umuhimu unaostahili.
“ Mkutano wa mwaka huu wa  Tume ya Umoja wa Mataifa kuhusu Hali ya Wanawake,  ni fursa nzuri ya  kufikia maamuzi ya pamoja    kati ya serikali  na Asasi zisizo za kiserikali kuhusu mikakati ambayo kweli inaweza kuleta  mabadiliko ya kweli kuhusu  maisha ya wanawake wa vijijini “. Akasititiza  Naibu Katibu Mkuu.
Kwa upande wake Waziri Sophia Simba akichangia majadiliano kuhusu  hali ya wanawake wa vijijini, ameeleza kwamba, Tanzania licha ya kuweka será na sheria zinazolenga kumsaidia mwanamke pia imeanzisha benki ya wanawake inayolenga kumkomboa kiuchumi  mwanamke akiwao yule wa kijijini.
Hata hivyo anasema ili será, na mipango iliyowekwa na serikali iweze kweli kumnufaisha mwanamke, ikiwamo  mpango mkakati wa Kilimo Kwanza, bado suala la elimu ni muhimu sana kwa wanawake.
Akasema ni kwa kupitia elimu ndipo kweli mwanamke hasa yule wa kijijini kwanza, anaweza kujitambua  yeyé ni  nani lakini pia ataweza kuzitumia fursa anazo pewa kikamilifu.
Akatoa mfano kwa kusema kuwa   katika kutambua umuhimu wa elimu si kwa wanawake tu, ndiyo maana serikali inaendelea kutekeleza   upelekaji wa elimu ya msingi hadi ngazi ya kila  kijiji na elimu  ya sekondari kwa kila kata.
“ wanawake wakiwa na elimu watakuwa na uelewa mpana wa kukabiliana na changamoto mbalimbali zikiwamo za kudhulumiwa mali zao , lakini watakuwa na fursa ya kufahamu namna bora ya kutumia  teknolojia za kisasa za kilimo, matumizi sahihi ya mitaji ya raslimali fedha na kubwa zaidi watajijengea  uwezo mkubwa wa  kupokea  na kuzitumia kikamilifu  na huduma mbalimbali  zinazolengwa kuwainua na kukabiliana na mfumo dume ” akasisitiza  Waziri  Sophia Simba.
Kuhusu namna gani Umoja wa Mataifa unaweza kushirikiana na serikali katika kuchagiza maendeleo ya wanawake. Waziri Simba ametoa wito wa taasisi hiyo ya kimataifa, kuhakikisha kwamba inafanya kazi kwa karibu na serikali   na kuzisaidia pale inapobidi kwa kusaidia uratibu na utekelezaji wa será, mipango na mikakati ambayo serikali inakuwa imejiwekea katika kuwakomboa na kuwaendeleza wanawake.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages