Breaking News

Your Ad Spot

Feb 24, 2012

MWILI WA MAMA WA BRANDINA NYONI NA JOHN BADI WA THIS DAY WAAGWA DAR


 Waombolezaji wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Esther Nyimbo Badi, katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Azania Front jijini Dar es Salaam, kabla ya mwili huo kusafirishwa kwenda Iringa kwa mazishi leo. Wakwanza kulia (waliosimama) ni mtoto wa marehemu, Brandina Nyoni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya ambaye kwa sasa amesimamishwa kazi hivi karibu kutokana na sakata la mgomo wa madaktari nchini.
 Jeneza lenye mwili wa marehemu likipakiwa kwenye gari tayari kwa safari kwenda Iringa
 Ndugu wa marehemu wakiwa na msalaba wakati wa kuga
Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye akijadiliana jambo na Mkuu wa Kanisa la KKKT Alex Malasusa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba Tanzania Nehemia Mchechu (kulia) wakati wa kuaga mwili wa marehemu Esther Nyimbo Badi, leo katika Kanisa la KKKT Azania Front, Dar es Salaam. leo. Marehemu Estether ni Mama mzazi Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Brandina Nyoni ambaye kwa sasa amesimamishwa kazi hivi karibu kutokana na sakata la mgomo wa madaktari. Kushoto ni Esther Sumaye
Mbunge wa Wawi (CUF) Hamad Rashid (kushoto) akibadilishana mawazo na baadhi ya waombolezaji wakati wa kuaga mwili wa marehemu Esther Nyimbo Badi, katika Kanisa la KKKT Azania Front, Dar es Salaam, leo. Baadhi ya waombolezaji hao ni Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadik na Waziri Wiliam Lukuvi. Estether ni Mama mzazi Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Brandina Nyoni ambaye kwa sasa amesimamishwa kazi hivi karibu kutokana na sakata la mgomo wa madaktari. Kushoto ni Esther Sumaye.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages