Breaking News

Your Ad Spot

Feb 25, 2012

RAIS KIKWETE ANG'ARISHA SHEREHE ZA MIAKA 50 YA CHAMA TAWALA CHA BOTSWANA LEO

Mgeni rasmi katika sherehe za miaka 50 ya chama tawala cha Botswana, Rais Jakaya Kikwete, akiwa na Rais wa Botswana Luteni Jenerali Seretse Khama Ian Khama, Makamuw a rais wa Afrika Kusini Bw Kgalema Nontlanthe, na Marais Wastaafu wa Botswana Sir Ketumile Masire ( wa pili shoto) na Bw Festus Mogae, wakijiandaa kukata keki ya sherehe hizo katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Botswana leo February 25, 2012

TAARIFA YA IKULU KUHUSU SHEREHE HIZO

DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
              press@ikulu.go.tz             

Fax: 255-22-2113425



PRESIDENT’S OFFICE,
      THE STATE HOUSE,
       P.O. BOX 9120,  
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais Jakaya Mrisho Kikwete amekipongeza Chama Tawala cha Botswana, Botswana Democratic Party (BDP) kwa mafanikio yaliyopatikana nchini Botswana na watu wake.

Rais Kikwete ametoa pongezi hizo katika Sherehe za Kuadhimisha Miaka Hamsini (50) ya Chama cha BDP  katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Botswana.
"Katika miaka hamsini ya uhai wake, BDP kimefanya mambo mengi mazuri nchini Botswana, katika ukanda huu na Afrika kwa ujumla na kimekuwa na historia nzuri ya kufanya mambo mengi mazuri ya kuvutia na kutolewa mfano barani kote" Rais amesema.

Rais Kikwete ametolea mfano wa Pato la ndani la Taifa la Botswana ambapo, wakati wa uhuru wa Botswana mwaka 1966, lilikuwa dola za kimarekani 70 tu, hadi kufikia dola za kimarekani 16,300 mwaka 2011.

"Haya ni mafanikio makubwa sana Barani Afrika" Rais amesema na kukipongeza kwa dhati Chama cha BDP ambacho kinatawala tangu uhuru wake.
Mapema akizungumza na wananchi Rais wa Botswana PM Gen. Seretse Khama Ian Khama ameeleza kuwa Tanzania imetoa mchango mkubwa na kuwa urafiki wa nchi mbili hizi ni wa kudumu.

"Tanzania imesimamia Uhuru, Haki na Ukweli barani Afrika" amesema na kueleza kuwa nchi yake itaendelea kusimamia na kuheshimu misingi hiyo.
Rais Khama pia amewakumbusha wanachama na wananchi wa Botswana kuwa umoja wao ndiyo ngao kubwa ya Chama cha BDP na kwamba chama hicho bado kiko imara kutokana na umoja wao huo na kinapania kuendeleza, kuuthamini na kuulinda Umoja wao.

Sherehe hizo zimehudhuriwa pia na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, Bwana Wilson Mukama.

Rais Kikwete anatarajiwa kurejea Dar-es-Salaam kesho tarehe 25 Februari, 2012. 
Mwisho.


Imetolewa na Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari Msaidizi wa Rais,
Gaborone, Botswana
24 Februari, 2012

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages