Breaking News

Your Ad Spot

Mar 13, 2012

CCM YAZINDUA KWA KISHINDO KAMPENI ZAKE ARUMERU

Mweneyekiti wa CCM na Rais Mstaafu Benjamin Mkapa akimnadi mgombea wa CCM Sioi Sumari kwenye alipozindua kampeni za CCM za uchaguzi mdogo jimbo la Arumeru Mshariki kwenye Uwanja wa mpira wa Ngaresero, Arumeru leo.
Mkapa akihutubia maelfu ya wananchi kwenye  mkutano huo
Katibu Mkuu wa CCM Wilson Mukama akimkaribisha Mkapa kuzindua kampeni hizo
Pamela Sioi Sumari akimnadi mumewe Sioi Sumari wakati wa uzinduzi wa kampeni hizo za CCM. Pamela ni mtoto wa Waziri Mkuu wa Zamani Edward Lowassa
Sioi akiomba kura kwa wananchi kwenye mkutano huo
Mratibu wa kampeni za CCM, ambaye ni Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha, Mwigulu Nchemba akihutubia wananchi kwenye mkutano huo.
William Sarakikya ambaye alichuana vikali katika kura za maoni kupata mgombea wa CCM, akimuombea kura Sioi kwenye mkutano huo
"Wenzetu alama yao ni kama kijiti hiki mnavyokiona!, achaneni nacho kitupeni, mpigieni kura Sioi alete maendeleo Arumeru." akasema Elirehema Kaaya ambaye naye 'alikula sahani moja' na Sioikwenye kura za maoni za CCM. Kushoto ni mratibu wa kampeni za CCM kitaifa Mwigulu Nchemba.
Kisha akaenda kumpa mkono wa pongezi Sioi kwa kupata ridhaa ya kupeperusha bendera ya CCM kwenye uchaguzu huo ambao utafanyika Aprili mosi mwaka huu.
Wanachama wa CCM wakishangilia kwa furaha Mkapa alipokuwa akimtambulisha na kumuombea kura mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM Sioi
Sehemu ya maelfu ya watu waliofurika uwanja wa Ngarosero wakati wa mkutano huo
Msafara wa waendesha pikipiki ukiongozwa na Mwigulu (katikati) na Katibu Mkuu wa Umoja wa vijana wa CCM, Martin Shigella wkati ukiingia kwenye uwanja wa Ngarosera kwenye uzinduzi wa kampeni hizo
Msafara huo ukila kona katikati ya mji mdogo wa Usa, wakati ukienda Uwanjanbi na kama kawaida wanaoongoza na Mwigulu na Shigela
Waednesha pikipiki wakipiga misele uwanjani
Mwanzo kabisa kulikuwa nba viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini wakiuombea dua njema mkutano. Pichani ni Mkapa na viongozi wa jukwaa kuu wakiwa wamesimama kupokea dua kutoka kwa mmoja wa viongozi a dini

Masanja Mkandamizaji akifanya machejo yake mbele ya umati wa watu waliohudhuria mkutano huo
Katika vimbwanga vyakeMasanja wa Orijino Komedi akabebana na Joti kama hivi ili mradi kunogesha burudani
Mmoja wa mashabiki wa CCM waliohudhuria mkutano huo akionyesha ukereketwa wake
Wananchi wakishangilia wakati msafara wa CCM ulipokuwa ukipita mtaani kwao ukiemda uwanjani kwenye mkutano huo
Sioi na mkewe wakiwa wamepumzika kabla ya kwenda mkutanoni

2 comments:

  1. Serwis posiada frikowe obrazy i filmiki z serii [url=http://www.szmule.pl]sex anonse[/url]. Galerie erotyczne przeznaczone jedynie dla widzow doroslych. Codzienna aktualizacja materialow. Zobacz juz dzis!

    ReplyDelete
  2. Drop in on us contemporary to come by more facts and facts in the matter of Come to see us at the moment to obtain more knowledge and facts anyway [url=http://www.kalendarze-ksiazkowe.net.pl]Kalendarze książkowe[/url]

    ReplyDelete

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages