Breaking News

Your Ad Spot

Mar 11, 2012

CCM YASEMA ITAZINDUA KAMPENI ZAKE KESHO KWA KISHINDO ARUMERU

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kesho Jumatatu, Machi 12, mwaka huu kitalitikisa jimbo la Arumeru Mashariki katika uzinduzi wa kampeni zake za uchaguzi mdogo wa jimbo hilo utakaofanywa na Mwenyekiti Mstaafu wa CCM, Rais Mstaafu Benjamin Mkapa.
Mwenyekiti Mstaafu, Benjamin Mkpa alitarajiwa kuwasili Arumeru Mashariki, jana jioni tayari kwa uzinduzi wa kampeni hizo.
Akizungumza jimboni hapa, Mratibu Kitaifa wa kampeni za CCM katika uchaguzi huo, Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha Mwigulu Nchemba alisema mkutano wa uzinduzi wa kampeni hizo utafanyika  Uwanja wa mpira wa Ngarasero na unatarajiwa kuhudhuriwa na maelefu ya watu kutokana na idadi kubwa ya wanachama na wapenzi wa CCM waliopo jimboni humo.
Mwigulu alisema watakaohudhuria mkutano huo wengi wanatarajiwa kutoka jimboni humo tofauti na CHADEMA ambao alidai katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni zao jana (juzi) walisomba kwa magari mamluki kutoka Moshi, Arusha mjini na maeneo mengine nje ya jmbo hilo.
Alisema shamra shamra za mkutano huo utakaofanyika saa tisa alasiri, zitaanza mapema kwa burudani zitakazotolewa na wasanii mbalimbali mahiri wakiongozwa na Kundi la Tanzania One Thetre (TOT Plus).
Akizungumzia kuhusu CHADEMA kulalamikia Tume ya Uchaguzi kuwa haitawatendea haki kwenye uchaguzi huo, Mwigulu alisema, hata safu yao ya uonozi tangu Mwekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe hadi wabunge ikishika nafasi zote kwenye Tume hiyo CCM lazima itashinda uchaguzi wa Arumeru Mashariki utakaofanyika Aprili Mosi mwaka huu.
"Kwa Uchaguzi huu wa Arumeru Mashariki, hata Katibu Mkuu wa CHADEMA Dk. Wilborod Slaa awe Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Mbowe (Mweyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe) awe Mkurugenzi wa Uchaguzi, Zitto (Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Kabwe Zitto) awe Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi  na wabunge wote  wa CHADEMA  wawe wasimamizi wa uchaguzi huo, halafu CCM tuweke mawakala tu, naapa kikwetu CCM itashinda", alisema Mwigulu.
Alisema malalamiko ya CHADEMA dhidi ya vyombo vitakavyosimamia uchaguzi huo ni woga wa kushindwa kwa sababu wanafahamu kuwa CCM imejiimarisha vya kutosha Arumeru Mashariki na italirejesha jimbo.

 

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages