Breaking News

Your Ad Spot

Mar 9, 2012

CHADEMA WAANZA KUMHOFU SIOI? WAMWELKEA PINGAMIZI

Tariifa kutoka Arumeru Mashariki tulizopata jioni hii zimesema CHADEMA kimemwekea pingamizi mgombea wa Ubunge jimbo hilo kwa tiketi ya CCM Sioi Sumari kwa madai kwamba si raia wa Tanzania.


Kwa mujibu wa habari hizo, CHADEMA wamedai kupata barua ya siri yenye Kumb/ No AR/C/32/VOL1/85, ya Feb 29/2/2012, kutoka kwa Ofisa Mfawidhi wa Uhamiaji mkoa wa Arusha, kwenda kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, ikifafanua uraia wa Sioi.


Inadaiwa katika barua hiyo ofisa huyo wa  uhamiaji  anaeleza kuwa,  yeyote aliyezaliwa nje ya nchi ukomo wa uraia wake unakomae anapofikisha miaka 18 na kwamba  baada ya hapo anapaswa kuukana uraia wa nchi alikozaliwa.


Kulingana  na madai hayo CHADEMA inataka ionekane kwamba kwa kuwa Sioi Sumari alizaliwa Kenya si raia wa Tanzania kwa kuwa hakuwahi kuomba uraia wa Tanzania.


Akizungumzia hatua hiyo, Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha Mwigulu Nchemba ambaye ndiye mratibu wa kampeni za CCM Kitaifa kwenye uchaguzi mdogo wa Arumeru Mashariki amebeza na kusema kwamba CHADEMA hawana hoja, ispokuwa wamefikia hatua hiyo kwa sababu wanajaribu kutafuta njia ya kupenya kwa sababu wanaogopa kubwagwa kwenye sanduku la kura.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages