Breaking News

Your Ad Spot

Mar 9, 2012

WAZIRI MALIMA AIBIWA HOTELINI MOROGORO

Adam Kighoma Malima

Naibu Waziri wa Nishati na Madini Adamu Kighoma Malima amekombwa  vitu vyake vyote vyenye thamani ya zaidi ya sh. milioni 15 katika hoteli ya kitalii ya Nashera ya mjini Morogoro.


Taarifa za kipolisi zilizopatikana kutoka mjini Morogoro  zimethibitisha kutokea wizi huo zikisema ulitokea usiku wa kuamkia leo.


Zilimkariri Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai  mkoa wa Morogoro,  Hamis Seleman taarifa zilmesema wizi umetokea wakati  waziri huyo alipokuwa  amejipumzisha  kwenye sebule ya chumba chake kwenye hoteli hiyo hadi  mida ya  10.45 ndipo alibaini kuibiwa vitu hivyo baada ya kurudi chumbani.


Kwa mujibu wa polisi  zimeibwa  fedha taslimu  Dola 4000 za Marekani na  Sh. milioni 1.5, pete mbili za silva zenye thamani ya sh. milioni 2, simu zenye thamani ya sh. milioni 1.3, balaghashia yenye thamani ya sh. 50,000, laptop mbili zenye thamani ya sh. milioni 5.6, taperecorder na headphone vyote vya sh. milioni moja.


Polisi wanasema dirisha la aluminium la chumba cha hoteli alimokuwa Malima limekutwa limevunjwa kwa kitu kigumu.


Habari zinasema nje ya dirisha hilo zimeoneka nyayo nje na ndani ya chumba jambo linaloashiria kuwa ni za mwizi.


Kufuatia wizi huo, walinzi watatu wa hotel hiyo wanashikiliwa na polisi huku taarufa zilizopatikana baadaye tukiandaa kurusha ripoti hii zikisema kwamba baadhi ya vitu vilivyoibwa vimepatikana, ingawa havikutajwa.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages