Breaking News

Your Ad Spot

Mar 27, 2012

MRADI WA MAJI WA VODACOM KUNUFAISHA WANAKIJIJI 4,000 DODOMA

Mwanamke akitishwa ndoo ya maji wakati wa uzinduzi wa mradi huo
Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania kupitia mfuko wake wa kusaidia Jamii (Vodacom Foundation) imekabidhi mradi wa maji wenye thamani ya shilingi milioni 40 katika kijiji cha Inyumbu ikiwa ni mwendelezo wa azma yake ya kusaidia jamii hapa nchini.

Kukabidhiwa kwa mradi huo kunapunguza shida ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kwa wakazi zaidi ya 4,000 wa kijiji cha Inyumbu na maeneo jirani.

Akipokea mradi huo Mwenyekiti wa Kijiji hicho Bw.Yona Ngobito aliishukuru kampuni ya Vodacom  kwa kuwekeza shilingi Milioni 40 ili kuokoa maisha ya wananchi ikifahamika wazi kuwa maji ni bidhaa muhimu na  nyeti katika maisha ya binadamu.

"Kila msaada ni muhimu kwa walengwa husika ila tunapozungumzia maji tunagusa moja kwa moja uhai wa binadamu, hili ni jambo jema kwenu wanakijiji wa Inyumbu ambao sasa wanawake na wasichana wanaweza kutumia muda mfupi kupata bidhaa hiyo na kutumia muda wa ziada kufanya shughuli nyengine za kifamilia"Alisema Mwenyekiti huyo.

Hata hivyo Mwenyekiti huyo wa kijiji ametumia pia fursa hiyo kuwasihi wanakijiji kuona thamani ya mradi huo na njia pekee ya kurudisha shukrani kwa Vodacom ni kuutunza mradi huo ili uwasidie kwa muda mrefu zaidi.

"Ndugu zangu hasa wakina mama tukitambua shida ambayo tulikuwa nayo hapo kabla ya kuletewa mradi huu na Vodacom ni wazi tutaona thamani yake na kila mmoja atakuwa mlinzi wa mradi huu dhidi ya aina yoyote ya uharibifu, hiyo si tu kwamba itatusaidia kuwa na uhakika wa maji bali tutawapa nguvu Vodacom kurudi tena kuangalia eneo jingine la kutusaidia"Aliongeza Ngobito.

Nae Mkuu wa kitengo cha Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule,alisema Vodacom Foundation imekua ikithamini maisha ya watanzania wengi na hivyo kujitolea katika kusaidia na kufadhili shughuli mbalimbali za maendeleo ya kijamii hapa nchini.

Aliongeza kuwa kutokana na kwamba Mkoa wa Dodoma una ukame katika baadhi ya maeneo yake na hivyo kuleta changamoto katika upatikanaji wa maji safi na salama kwamatumizi ya binadamu hasa maeneo ya vijijini jambo lililoigusa kampuni ya Vodacom kupitia mfuko huo na kufikia uamuzi wa kufadhili mradi huo wa maji kupitia teknolojia ya upepo.
.
"Katika jitihada zetu za kuboresha ustawi wa jamii za watanzania kwa kuwa washirika wa huduma za kijamii nchini zimetufikisha hapa katika kijiji cha Inyumbu kukabidhi mradi huu, ni matumaini yangu kwamba sasa mama zangu wa hapa kijijini wamefurahi kwa kupunguziwa hali iliyokwepo hapo  awali ya kutumia muda mrefu kusaka maji kwa shughuli mbalimbali za kifamilia"Alisema Mwakifulefule.

Kila mwaka tunatenga fedha kusaidia maeneo mbalimbali ya kijamii hasa elimu,afya, maji,mazingira na ujasiriamali, tunafanya hivyi tukitambua kuwa biashara kwetu ni sehemu moja ila namna tunavyokuwa karibu kusaidia wale wanaotuzunguka katika baishara zetu ni jambo moja muhimu sana katika shughuli zetu, tutaendelea kufanya hivyo tukiamini kwamba azma yetu ya kubadili maisha ya wananchi inatekelezeka"Aliongeza Mwakifulefule.

Vodacom kupitia Vodacom Foundation iliufandhili mradi huo kwa shilingi Milioni 40 kupitia Mamlaka ya maji ya kijiji cha Inyumbu kwa kushirikiana na mradi wa maji wa C.P.P.S,

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages