ZANZIBAR
Mohammedraza Dharamsi aliyekuwa mwakilishi mteule jimbo la Uzini, leo ameapishwa rasmi na Spika wa Baraza la Wawakilishi, Pandu Ameir Kificho tayari kushika mikoba ya kuongoza jimbo hilo.
Mohammedraza maarufu kama Raza aliapishwa leo asubuhi mida ya saa nne asubuhi, katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi.
Raza ametinga Barazani baada ya kuibuka na ushindi mkubwa katika uchaguzi mdogo uliofanyika mwezi uliopita ambapo alipata ushindi wa asilimia 61.
Akizungumza baada ya kuapishwa Raza amewashukuru wananchi wa Uzini kwa kumwamini na hatimaye kumchagua kuwa mwakilishi wao.
"Sina cha kusema zaidi lakini nawashukuru wananchi wa Uzini kwa kuniamini na kunipa dhamana hii kubwa ya kuwaongoza hivyo naamini sitawaangusha,''alisema.
Alisema wakati wa mchakato wa kupata jina la moja la mgombea ndani ya chama walikuwa 14 huku kati yao 13 wakiwa wazawa wa jimbo hilo na mmoja(yeye) akiwa si mzawa.
"Licha ya kuwepo na wazawa wa jimbo hilo, bado wanachama na baadae wananchi wa Uzini walinihitaji mimi kuwa mwakilishi wao kwa kuwa naweza kuwatumikia kwa moyo mkunjufu,''alisema.
Katika kudhihirisha furaha yake, Raza amesema mshahara wake wa kila mwezi atautoa kwa wananchi wa jimbo hilo kutekeleza miradi ya maendeleo akisema anafanya hivyo kwa sababu hakuihitaji nafasi hiyo kwa ajili ya kuganga njaa bali kusaidia wananchi.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269